{"id":20458,"date":"2023-05-18T12:06:48","date_gmt":"2023-05-18T12:06:48","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=20458"},"modified":"2023-07-13T08:21:40","modified_gmt":"2023-07-13T08:21:40","slug":"bayatul-aqabah-kiapo-cha-ahadi-ya-utii-cha-kwanza","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/bayatul-aqabah-kiapo-cha-ahadi-ya-utii-cha-kwanza\/","title":{"rendered":"BAY&#8217;ATUL AQABAH KIAPO CHA AHADI YA UTII CHA KWANZA"},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Tumetaja kuwa watu sita miongini mwa watu wa Yath&#8217;tib (Madina) walisilimu katika msimu wa Hijja mnamo mwaka wa kumi na moja wa Utume na waliweka ahadi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) kuwa watafikisha ujumbe wake kwa jamaa zao Madina. Kutokana na ahadi hiyo msimu uliofuata wa mwaka wa kumi na mbili wa Utume, mnamo mwezi wa Julai mwaka wa <span style=\"color: #ff6600;\">621 C.E,<\/span> walikuja watu kumi na wawili miongoni mwao walikuwemo watu watano katika wale waliougana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) mwaka uliotangulia, mtu wa sita ambaye hakuhudhuria ni J<span style=\"color: #ff6600;\">abir bin Abdillah bin Riab.<\/span> Watu saba wengine walikuwa ni:-<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">1.<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Muadh bin Al-Harith Ibni Afraa<\/span> kutoka katika kabila la BanuAn-Najar Katika Khazraji).<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">2.<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Dhakwan bin Abdi Al-Qays<\/span> kutoka Banu Zuraiq (katika Khazraji)<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">3.<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Ubada bin Swamiti,<\/span> kutoka Banu Ghanani (katika Khazraji)<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">4. Yazidi bin Tha\u2019alaba,<\/span> katika marafiki wa Banu Ghanam (katika Khazraji)<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">5.<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Al Abbas bin \u2019Ubada bin Fadhlah<\/span> katika Banu Salim, (katika Khazraji)<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">6. Abu Haytham bin Tayhani<\/span> katika Banu Ash-hal (katika Ausi)<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">7. Uwaym bin Saidah kutoka Banu Amri bin Aufi<\/span> (katika Ausi) wawili katika hao ni katika Ausi na waliobaki wote ni katika Khazraj&#8217;<\/p>\n<p>Watu hawa wote waliungana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) Aqabah huko Mina. Wakamwahidi Bay&#8217;atu An Nisaa, ni sawasawa na ile ahadi ya wanawake ambayo ilishuka wakati wa Fathu Makka.<\/p>\n<p>Bukhari amepokea kutoka kwa \u2019Ubada bin Swamiti kuwa Mtume (\ufdfa) alisema,<\/p>\n<p style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0628\u064e\u0627\u064a\u0650\u0639\u064f\u0648\u0646\u0650\u064a \u0639\u0644\u064e\u0649 \u0623\u0646\u0652 \u0644\u0627 \u062a\u064f\u0634\u0652\u0631\u0650\u0643\u064f\u0648\u0627 \u0628\u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u0650 \u0634\u064a\u0626\u064b\u0627\u060c \u0648\u0644\u064e\u0627 \u062a\u064e\u0633\u0652\u0631\u0650\u0642\u064f\u0648\u0627\u060c \u0648\u0644\u064e\u0627 \u062a\u064e\u0632\u0652\u0646\u064f\u0648\u0627\u060c \u0648\u0644\u064e\u0627 \u062a\u064e\u0642\u0652\u062a\u064f\u0644\u064f\u0648\u0627 \u0623\u0648\u0652\u0644\u064e\u0627\u062f\u064e\u0643\u064f\u0645\u0652\u060c \u0648\u0644\u064e\u0627 \u062a\u064e\u0623\u0652\u062a\u064f\u0648\u0627 \u0628\u0628\u064f\u0647\u0652\u062a\u064e\u0627\u0646\u064d \u062a\u064e\u0641\u0652\u062a\u064e\u0631\u064f\u0648\u0646\u064e\u0647\u064f \u0628\u064a\u0652\u0646\u064e \u0623\u064a\u0652\u062f\u0650\u064a\u0643\u064f\u0645\u0652 \u0648\u0623\u064e\u0631\u0652\u062c\u064f\u0644\u0650\u0643\u064f\u0645\u0652\u060c \u0648\u0644\u064e\u0627 \u062a\u064e\u0639\u0652\u0635\u064f\u0648\u0627 \u0641\u064a \u0645\u064e\u0639\u0631\u0648\u0641\u064d\u060c \u0641\u0645\u064e\u0646 \u0648\u0641\u064e\u0649 \u0645\u0650\u0646\u0643\u064f\u0645 \u0641\u0623\u062c\u0652\u0631\u064f\u0647\u064f \u0639\u0644\u064e\u0649 \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u0650\u060c \u0648\u0645\u064e\u0646 \u0623\u0635\u064e\u0627\u0628\u064e \u0645\u0650\u0646 \u0630\u0644\u0643\u064e \u0634\u064a\u0626\u064b\u0627 \u0641\u064e\u0639\u064f\u0648\u0642\u0650\u0628\u064e \u0641\u064a \u0627\u0644\u062f\u0651\u064f\u0646\u0652\u064a\u064e\u0627 \u0641\u064e\u0647\u0648 \u0643\u064e\u0641\u0651\u064e\u0627\u0631\u064e\u0629\u064c \u0644\u0647\u060c \u0648\u0645\u064e\u0646 \u0623\u0635\u064e\u0627\u0628\u064e \u0645\u0650\u0646 \u0630\u0644\u0643\u064e \u0634\u064a\u0626\u064b\u0627 \u062b\u064f\u0645\u0651\u064e \u0633\u064e\u062a\u064e\u0631\u064e\u0647\u064f \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064f \u0641\u064e\u0647\u0648 \u0625\u0644\u0649 \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u0650\u060c \u0625\u0646\u0652 \u0634\u064e\u0627\u0621\u064e \u0639\u064e\u0641\u064e\u0627 \u0639\u0646\u0652\u0647 \u0648\u0625\u0646\u0652 \u0634\u064e\u0627\u0621\u064e \u0639\u064e\u0627\u0642\u064e\u0628\u064e\u0647\u064f \u0641\u064e\u0628\u064e\u0627\u064a\u064e\u0639\u0652\u0646\u064e\u0627\u0647\u064f \u0639\u0644\u064e\u0649 \u0630\u0644\u0643\u064e.<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"> \u201dNjooni, nipeni ahadi ya kuwa hamtakishirikisha kitu chochote na Mwenyezi Mungu (s.w.t), hamtaiba, hamtazini, hamtawaua watoto wenu na hamtauleta uzushi ambao mtauzua kati ya mikono yenu na miguu yenu na kuwa hamtaniasi katika maamrisho ya kutenda mema. Atakayetekeleza haya miongoni mwenu malipo yake yako kwa Allah (s.w.t) na atakayetenda jambo katika mambo hayo ataadhibiwa hapa duniani, kuadhibiwa huko kutakuwa ni kafara kwake na atakayetenda jambo katika mambo hayo na Mwenyezi Mungu (s.w.t) Akamsitiri, basi jumbo lake Mwenyezi Mungu Atalisitiri, Akitaka Atamuadhibu na Akitaka Atamsamehe. \u201d Akasema, \u201dNikampa ahadi.\u201d Na pahala pengine imesemwa, \u201dTukula kiapo juu ya hilo.<\/span> (1) .<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>BALOZI WA UISLAMU MADINA<\/strong><\/span><\/p>\n<p>Baada ya kutimia kiapo cha ahadi ya utii kwa Mtume (\ufdfa) na msimu ukamalizika, Mtume (\ufdfa) alimpeleka pamoja na hawa waumini walioweka ahadi Balozi wa kwanza huko Yathri&#8217;b. Pamoja na &#8216;kazi nyingine, awafundishe Waislamu Sheria za Kiislamu na awafahamishe Dini, pamoja na kusimama kueneza Uislamu kati ya wale ambao bado ni Washirikina. Aliyechaguliwa kuwa Balozi ni kijana katika vijana wa Kiislamu, <span style=\"color: #ff6600;\">Mus&#8217;ab bin \u2019Umair Al-Abdary<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake).<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>MAFANIKIO YANAYOFURAHISHA.<\/strong> <\/span><\/p>\n<p>Mus&#8217;ab bin &#8216;Umair (Radhi za Allah ziwe juu yake) ali\ufb01kia kwa<span style=\"color: #ff6600;\"> Asiad bin Zurarah<\/span> na kwa pamoja wakawa wanautangaza Uislamu kwa watu wa Yathrib kwa jitihada na hamasa. <span style=\"color: #ff6600;\">Mus&#8217;ab akapewa jina la Al- Muqriu<\/span> (yaani msomeshaji wa Qur&#8217;an). Miongoni mwa mambo ya kufurahisha yaliyopokewa katika kufanikiwa kwa Mus&#8217;ab (Radhi za Allah ziwe juu yake) katika kazi yake ya Da\u2019awa ni kuwa, siku moja alitoka na <span style=\"color: #ff6600;\">Asiad bin Zurarah<\/span> kuelekea nyumba za Banu <span style=\"color: #ff6600;\">Abdil Ashhal na Banu Dhafar.<\/span> Wakaingia katika moja ya bustani miongoni mwa mabustani ya Banu Dhafar wakakaa kando ya kisima kinachoitwa <span style=\"color: #ff6600;\">Biiru Maraq<\/span> \u2014 Waislamu wengi walikusanyika hapo (wakati Sa&#8217;ad bin Muadh na Usaid bin Khudhair waliokuwa mabwana miongoni mwa jamaa zao katika Banu Abdi Ashhal bado ni Washirikina). Walipolisikia jambo hilo, Sa\u2019ad alisema kumwambia Usaid, \u201dNenda kwa hawa watu wawili ambao inaelekea kuwa wamekuja ili kuwafanya wapumbavu watu wetu na ukawakemee na kuwakataza wasifike nyumbani kwetu, maana <span style=\"color: #ff6600;\">Asad bin Zurarah<\/span> ni mtoto wa mama yangu. mkubwa na laiti isingelikuwa hivyo, ningelikwenda kumzuia mweny\u00e9we.\u201d Usaid akachukua sime yake, na akawafuata, Asad alipomwuona aliwambia Mus\u2019ab (Radhi za Allah ziwe juu yake), &#8220;HIuyo ni kiongozi wa jamaa zako amekufuata, mwambie ukweli kuhusu Mwenyezi Mungu (s.w.t).&#8221; <span style=\"color: #ff6600;\">Mus\u2019ab<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) akasema, \u201dIwapo atakaa nitamsemesha.\u201d &#8216;<span style=\"color: #ff6600;\">Usaid<\/span> akafika na huku akitoa matusi na kuhoji ni jambo gani lililowaleta kwetu? Kwa nini mnawafanya watu wetu kuwa ni wapumbavu, ondokeni kama mnahaja na nafsi zenu; <span style=\"color: #ff6600;\">Mus\u2019ab<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) akamwambia, \u201dKwa nini usikae na kusikiliza ujumbe tulionao, kama utaridhika na jambo lolote utalikubali na kama utalichukia utaliacha na kufanya hivyo ndiyo uadilifu, akakubali, akaichomeka chini sime yake na kukaa.\u201d<span style=\"color: #ff6600;\"> Mus\u2019ab<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) akaanza kumuelezea kuhusu Uislamu na mwisho akamsomea Qur&#8217;ani.<\/p>\n<p>Baada ya kuisikiliza alisema, &#8220;Ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa hakika tuliujua usoni mwake Uislamu kabla hajasema kutokana na kumeremeta na kumemetuka kwake\u201d; Kisha akasema, <em>\u201cNi uzuri ulioje wa aya hizo na ubora wake?<\/em>\u2019 Aliuliza, <em>\u201d]e, Mtu akitaka kuingia katika dini hii anafanyaje?<\/em> Akaelezwa; \u201dUtaoga, na kuzitakasa nguo zako, kisha utashuhudia Shahada ya ukweli, kisha utasali rakaa mbili.\u201d Akasimama, akaoga na kuzizitakasa nguo zake na akatamka Shahada na akasali rakaa mbili. Baada ya hapo akasema,<em> &#8220;Kwa hakika nyuma yangu yupo mtu, mtu huyu akiwafuateni basi hatabaki nyuma mtu yeyote katika jamaa zake na hivi ninakwenda kumleta kwenu hivi sasa.\u201d<\/em> Akaichukua sime yake na akaenda kwa Sa\u2019ad na akamkuta amekaa katika jumba lao la mikutano akiwa na jamaa zake. Sa\u2019ad alipomuona akasema, <em>\u201cNinaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu jamaa yenu anawajieni na uso tofauti na ule ambao alikwenda nao kutoka kwenu.\u201d<\/em> Usaid alisimama katikati ya Jumba la mikutano na kumuuliza Sa&#8217;ad, \u201dUmefanya nini?.\u201d Akajibiwa; \u201dNimesema na wale watu, lakini ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu sikuwakuta na ubaya wowote na kwa hakika niliwakataza, lakini wakasema, Tutafanya lile ambalo unalipenda, na kwa hakika nimeelezwa kuwa <span style=\"color: #ff6600;\">Banu Haritha<\/span> wametoka kwenda kwa <span style=\"color: #ff6600;\">As&#8217;ad bin Zurarah<\/span>, ili wakamuue &#8211; na hilo ni kwa sababu yeye ni mtoto wa mama yako mkubwa ili waivunje ahadi yako.\u201d Sa\u2019ad akasimama hali ya kuwa ameghadhibika kwa sababu ya lile aliloambiwa, akachukua sime yake na akatoka kuwafuata na alipowaona walivyotulizana Usaid alielewa kuwa kwa hakika hakuna vinginevyo isipokuwa alitakiwa awasikilize. Aliwasimamia huku akitoa matusi na kupaza sauti, \u201dNinaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ewe Aba Umama, laiti kama isingelikuwa kwa udugu tulionao usingelithubutu kulifanya jambo hili kwangu, katika majumba yetu na yale ambayo tunayachukia? Mus\u2019ab (Radhi za Allah ziwe juu yake) akakumbuka maneno aliyoambiwa na As&#8217;ad kuwa, \u201dHuyu ni Bwana ambaye nyuma yake pana jamaa wengi, iwapo atakufuata hatabaki nyuma yoyote katika wao.\u201d Akasema kumwambia Sa\u2019ad bin Muadh, <em>\u201dHivi huwezii kukaa ili usikilize? Kama utaliridhia jambo utalikubali na iwapo utalichukia tutaliondoa lile ambalo unalichukia.&#8221;<\/em> Akasema, \u201dKwa hilo umefanya uadilifu\u201d, akaichomeka chini sime yake na akakaa ili kusikiliza. Mus&#8217;ab (Radhi za Allah ziwe juu yake) akamfahamisha kuhusu Uislamu na mwisho akamsomea Qur\u2019an, alisema, tukaujua katika uso wake Uislamu kabla hajatamka kutokana na kukunjuka kwake na kumeremeta kwake, na kisha akauliza,<em> \u201dHuwa mmnafanya nini mtu anapotaka kusilimu?<\/em> Wakamfahamisha; \u201dUtaoga na utazitakasa nguo zako, kisha utashuhudia Shahada ya kweli na baada ya hapo utasali rakaa mbili.&#8221; Akafanya kama alivyoelekezwa na baadaye akachukua sime yake na kurudi kwenye Jumba la Mikutano kwa jamaa zake, walipomwona tu walisema; <em>\u201dTunaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu amerudi na uso tofauti na ule ambao alikwenda nao.&#8221;<\/em> Alipofika na kusimama mbele yao aliwauliza; <em>&#8220;Enyi Banu Abdil Ashhal mimi mnanifahamu kwa sifa ipi kwenu?&#8217;<\/em> Wakamjibu, \u201dWewe ni Bwana wetu na ni mbora wetu kwa maoni na mwema wetu zaidi kwa tabia.\u201d Akasema; &#8220;Kwa hakika kuanzia sasa maneno ya wanaume wenu na wanawake wenu kwangu ni haramu mpaka mumwamini Mwenyezi Mungu (s.w.t) na Mtume wake (\ufdfa).\u201d Jua halikuchwa siku hiyo isipokuwa wote wanaume na wanawake miongoni mwao walikuwa tayari wamekwisha kuwa Waislamu, isipokuwa mtu mmoja aliyekuwa akiitwa Al- Uswairim huyu alichelewa kusilimu mpaka siku ya vita vya Uhud. Aliposilimu tu aliingia vitani na kuuawa, hakuwahi kumsujudia Mwenyezi Mungu (s.w.t) sijida yoyote, kuhusu mtu huyu Mtume (\ufdfa) alisema, <span style=\"color: #0000ff;\">\u201dAmetenda kidogo na amelipwa sana. &#8221; <\/span><\/p>\n<p>Mus&#8217;ab (Radhi za Allah ziwe juu yake) alifanya makazi yake katika nyumba ya <span style=\"color: #808000;\">As&#8217;ad bin Zurarah,<\/span> akiwalingania watu kwenye Uislamu. Haikubaki nyumba yoyote katika nyumba za Answari isipokuwa ndani yake mlikuwa na wanaume na wanawake ambao tayari walikuwa wamekwisha ingia katika Uislamu, isipokuwa nyumba ya <span style=\"color: #ff6600;\">Banu Umayyah bin Zaid, Khatma na Wail,<\/span> ambao walikuwa wakikaa na <span style=\"color: #ff6600;\">Qais bin Aslat,<\/span> mshairi waliyekuwa wakimtii ambaye aliwachelewesha kuingia katika Uislamu mpaka mwaka wa Khandaq, mwaka wa tano baada ya Hijra, kabla ya kuingia msimu wa Hijja iliyofuata. Katika mwaka wa kumi na tatu, <span style=\"color: #ff6600;\">Mus&#8217;ab bin Umair<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) alirudi Makka kumpelekea Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) khabari njema za mafanikio na akamsimulia khabari za makabila ya Yathrib na vipaji mbalimbali vya kheri walivyonavyo na mambo mengine katika uwezo wa nguvu na misimamo thabiti.<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1) Sahihil Bukhari, Iuzuu 1, Uk. 7, 550-551; Iuzuu 2, uk. 727, 1003.<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>2) Ibn Hisham, Iuzuu 1, Uk. 435-438; Iuzuu 2, Uk. 90. Zaad Ma&#8217;ad, luzuu 2, Uk.51.<\/em><\/span><\/div>\n<div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>*) Arrahiq Al-Makhtuum Uk -257-264<\/em><\/span><\/div>\n<\/div>\n<hr \/>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Tumetaja kuwa watu sita miongini mwa watu wa Yath&#8217;tib (Madina) walisilimu katika msimu wa Hijja mnamo mwaka wa kumi na moja wa Utume na waliweka ahadi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) kuwa watafikisha ujumbe wake kwa jamaa zao Madina. Kutokana na ahadi hiyo msimu uliofuata wa mwaka wa kumi na mbili wa [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-20458","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/20458","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=20458"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/20458\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":21304,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/20458\/revisions\/21304"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=20458"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=20458"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=20458"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}