{"id":19517,"date":"2023-02-23T10:35:26","date_gmt":"2023-02-23T10:35:26","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=19517"},"modified":"2023-03-09T12:25:24","modified_gmt":"2023-03-09T12:25:24","slug":"daawa-kwa-makabila-na-mtu-mmoja-mmoja","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/daawa-kwa-makabila-na-mtu-mmoja-mmoja\/","title":{"rendered":"DA&#8217;AWA KWA MAKABILA NA MTU MMOJA MMOJA"},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Katika mwezi wa Dhul Qa&#8217;dah katika mwaka wa kumi wa Utume, mwishoni mwa mwezi wa Juni na Julai mwaka wa 619 C.E. Mtume wa Mwenyezi Mung-u (\ufdfa) alirejea Makka kwa lengo la kuanza upya kuutangaza Uislamu miongoni mwa makabila, na kwa mtu mmoja mmoja. Kwa vile msimu wa Hijja ulikuwa ukikaribia watu walikuwa wanaanza kuja Makka kwa wingi, wengine kwa miguu &#8216;na wengine kwa wanyama wa kila aina wanaopandwa, kutoka katika miji ya mbali, kwa madhumuni ya kutekeleza ibada zao za Hijja na kufanya biashara, katika masiku yaliyokuwa yakijulikana.<\/p>\n<p>Mtume (\ufdfa) aliinyakua fursa hii na akaitumia kwa kuwaendea kabila baada ya kabila, akiwaita kwenye Uislamu kama alivyokuwa akifanya tokea mwaka wa nne wa Utume.<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>Makabila Aliyoyatangazia Uislamu.<\/strong><\/span><\/p>\n<p>Al-Zahry amesema tumejulishwa kuwa, miongoni mwa makabila ambayo Mtume (\ufdfa) aliyaendea na kuyaita na akajidhihirisha kwao ni <span style=\"color: #ff6600;\">Banu \u2019Amir bin Swaa Swaa<\/span>, <span style=\"color: #ff6600;\">Muharib bin Khafswa<\/span>, <span style=\"color: #ff6600;\">Fazara<\/span>, <span style=\"color: #ff6600;\">Ghassan<\/span>, <span style=\"color: #ff6600;\">Murra<\/span>, <span style=\"color: #ff6600;\">Hanifa<\/span>, <span style=\"color: #ff6600;\">Sulaym<\/span>, <span style=\"color: #ff6600;\">Absi<\/span>, <span style=\"color: #ff6600;\">Banu Nassr<\/span>, <span style=\"color: #ff6600;\">Banu Al-Bukaa<\/span>,<span style=\"color: #ff6600;\"> Kinda<\/span>, <span style=\"color: #ff6600;\">Kalb<\/span>, <span style=\"color: #ff6600;\">Al-Harithi bin Ka\u2019ab<\/span>, \u2019<span style=\"color: #ff6600;\">Udhrah na Al-Hadha\u2019rima<\/span>, lakini hakuna hata mtu mmoja aliyeitikia wito wa Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) miongoni mwao (1)<\/p>\n<p>Makabila haya yalitangaziwa Uislamu kuanzia mwaka wa nane wa Utume mpaka msimu wa mwisho kabla ya Hijra. Haiwezekani kutaja mwaka maalum wa kutangazwa Uislamu kwa makabila yote.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">Al-Mansour<\/span> aliye mwanachuoni mkubwa anaeleza kuwa yapo makabila ambayo kutangazwa kwa Uislamu kwao kulifanyika katika msimu wa mwaka wa kumi. (2)<\/p>\n<p>Kwa hakika <span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Ishaq<\/span> ameelezea namna alivyokuwa anawalingania na majibu yao, hapa tutataja maelezo hayo kwa ufupi: &#8211; .<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>1) Banu Kalb:<\/strong><\/span> inaelezwa kuwa Mtume (\ufdfa) alikwenda katika kabila moja miongoni mwao wanaoitwa<span style=\"color: #ff6600;\"> Banu Abdillah<\/span> akawalingania kumfuata Mwenyezi Mungu (\ufdfb) na akaonesha kwao nia yake njema kiasi chakuwaambia; <em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dEnyi Banu Abdillah kwa hakika Mwenyezi Mungu (\ufdfb) Amelzfanya zuri jinn la baba yenu.\u201d<\/span><\/em> Lakini hawakukubali kamwe kuliamini lile alilokuwa akiwatangazia.<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>2) Banu Hanifa:<\/strong> <\/span>Alikuwa akiwafuata katika majumba yao na kuwalingania katika kumtii na kumfuata Mwenyezi Mungu (\ufdfb) na akawathibitishia nia njema aliyokuwa nayo kwao. Lakini hakukuwahi kutokea watu miongoni mwa Waarabu waliokuwa na majibu mabaya sana kwake kuliko wao.<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>3) Banu &#8216;Amir bin Swaa Swaa:<\/strong><\/span> Mtume wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) alikwenda kwao na kuwalingania kumtii na kumfuata Mwenyezi Mungu (\ufdfb) na akawadhihirishia nia njema aliyo kuwa nayo kwao. <span style=\"color: #ff6600;\">Bahira bin Firas<\/span> (mtu mmoja miongoni mwao) akasema, \u201dNinaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu laiti kama mimi ningemkamata Kijana huyu, Makuraishi wangenila kwa sababu yake\u201d; kisha akasema; \u201d]e, unaonaje iwapo sisi tutakupa ahadi juu ya mambo yako\u201d, kisha Mwenyezi Mungu (\ufdfb) Akakupa ushindi dhidi ya wale ambao wanakupinga, jambo hilo litakuwa ni letu baada yako? \u00a0\u201d Akawajibu; <em><span style=\"color: #0000ff;\">&#8220;Jambo ni la Mwenyezi Mungu analiweka\u00a0 Annpopataka.&#8221;<\/span><\/em> Wakamwambia, \u201dHivi itakuaje sisi tujitolee mhanga kwa ajili yako na baada ya kupata ushindi watu wengine waliteke? Hatuna haja na jambo lakk.&#8221; Hivyo wakaukataa wito wake.<\/p>\n<p>Wakati <span style=\"color: #ff6600;\">Banu \u2019Amir<\/span> waliporejea kwao, walizungumza na mzee wao ambaye hakwenda Makka msimu huo, kwa sababu ya umri wake mkubwa, wakamweleza; \u201dAmetujia Kijana wa Kikuraishi kutoka katika kabila la Banu Abdil Muttwalib, anadai kuwa yeye ni \u2018 Mtume, anatulingania kwenye kumnusuru na anatutaka tusimame nae pamoja na tutoke nae kwenda kwenye miji yetu.\u201d Alipoyasikia maneno hayo yule mzee akaweka mikono yake juu ya kicnwa chake, na kisha akauliza; \u201dJe jambo hilo lina nafsi ya kudirikiwa?, Je, linaweza kutafutwa na kufuatiliwa baada ya kuponyoka? Ninaapa kwa yule ambaye nafsi ya fulani imo mikononi mwake, haijapata kutokea kutoka kwa watoto wa Ismail .(Alayhi salaam) mtu kudai Utume na kama ni hivyo kwa hakika huo Utume hi jambo la kweli, ni yepi yalikuwa maoni yenu kwake?.&#8221; (3)<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1) Ttirmidhy. Mukhtasar Siratu Rrasul, Uk. 149\u0632<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>2) Rahmatun Lil &#8216;Alamin, Iuzuu 1, Uk. 74. Tarikhul Islam, Iuzuu 1, Uk. 125<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>3) lbn Hisham, Iuzuu 1, Uk. 424-425.\u00a0<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>*) Arrahiq Al-Makhtuum Uk 235-237<\/em><\/span><\/div>\n<hr \/>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Katika mwezi wa Dhul Qa&#8217;dah katika mwaka wa kumi wa Utume, mwishoni mwa mwezi wa Juni na Julai mwaka wa 619 C.E. Mtume wa Mwenyezi Mung-u (\ufdfa) alirejea Makka kwa lengo la kuanza upya kuutangaza Uislamu miongoni mwa makabila, na kwa mtu mmoja mmoja. Kwa vile msimu wa Hijja ulikuwa ukikaribia watu walikuwa [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-19517","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/19517","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=19517"}],"version-history":[{"count":6,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/19517\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":19612,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/19517\/revisions\/19612"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=19517"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=19517"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=19517"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}