{"id":19212,"date":"2023-01-26T11:35:26","date_gmt":"2023-01-26T11:35:26","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=19212"},"modified":"2023-02-02T12:08:08","modified_gmt":"2023-02-02T12:08:08","slug":"kufariki-kwa-bi-khadija-radhi-za-allah-ziwe-juu-yake","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/kufariki-kwa-bi-khadija-radhi-za-allah-ziwe-juu-yake\/","title":{"rendered":"KUFARIKI KWA BI KHADIJA (Radhi za Allah ziwe juu yake)"},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Baada ya kufariki kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Twalib,<\/span> kwa kiasi cha miezi miwili au mitatu (na hapa pana kauli mbili zinazotofautiana) alifariki dunia mama wa waumini Bi <span style=\"color: #ff6600;\">Khadija Al-Kubra<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake). Alifariki mnamo mwezi wa Ramadhani, mwaka wa kumi wa Utume, akiwa na umri wa miaka sitini na tano na Mtumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) akiwa na umri wa miaka khamsini.<\/p>\n<p>Kwa hakika <span style=\"color: #ff6600;\">Bi Khadija<\/span> (Radhi za Allahziwe juu yake) alikuwa ni moja kati ya neema za Mwenyezi Mungu Zilizotukufu kwa Mtume wake (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>). Naye aliishi na Mtume (\ufdfa) kwa wema, muda mrefu. Akimhurumia wakati wa kukerwa kwake, akimsaidia katika nyakati zake za matatizo na alimsaidia pia katika kuu\ufb01kisha ujumbe wake. Alishirikiana naye katika gharama za jihadi yenye uchungu na alimliwaza kwa nafsi yake na mali zake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alisema;<\/p>\n<p style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0642\u062f \u0622\u0645\u064e\u0646\u064e\u062a\u0652 \u0628\u064a \u0625\u0630 \u0643\u0641\u064e\u0631\u064e \u0628\u064a \u0627\u0644\u0646\u0627\u0633\u064f\u060c \u0648\u0635\u062f\u0651\u064e\u0642\u064e\u062a\u0652\u0646\u064a \u0625\u0630 \u0643\u0630\u0651\u064e\u0628\u064e\u0646\u064a \u0627\u0644\u0646\u0627\u0633\u064f\u060c \u0648\u0648\u0627\u0633\u064e\u062a\u0652\u0646\u064a \u0628\u0645\u0627\u0644\u0650\u0647\u0627 \u0625\u0630 \u062d\u0631\u064e\u0645\u064e\u0646\u064a \u0627\u0644\u0646\u0627\u0633\u064f\u060c \u0648\u0631\u0632\u064e\u0642\u064e\u0646\u064a \u0627\u0644\u0644\u0647\u064f \u0639\u0632\u0651\u064e \u0648\u062c\u0644\u0651\u064e \u0648\u0644\u064e\u062f\u064e\u0647\u0627 \u0625\u0630 \u062d\u0631\u064e\u0645\u064e\u0646\u064a \u0623\u0648\u0644\u0627\u062f\u064e \u0627\u0644\u0646\u0651\u0650\u0633\u0627\u0621\u0650<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[ Aliniamini wakati watu waliponikufuru, alinisadikisha wakati watu waliponikadhibisha, alinishirkisha katika mali yake wakati watu waliponinyima na Mwenyezi Mungu Ameniruzuku mimi watoto kutoka kwake, na Hakunipa kutoka kwa asiyekuwa yeye ]<\/span> (1)<\/p>\n<p>Imepokewa katika hadithi sahihi kutoka kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Huraira<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa alisema: Jibril (Alayhi salaam) alimshukia Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) na akamueleza,<\/p>\n<p style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u064a\u0627 \u0631\u0633\u0648\u0644\u064e \u0627\u0644\u0644\u0647\u0650 ! \u0647\u0630\u0647\u0650 \u062e\u064e\u062f\u064a\u062c\u0629\u064f \u0642\u062f \u0623\u064e\u062a\u064e\u062a\u0652\u0643\u064e \u0645\u0639\u0647\u0627 \u0625\u0646\u0627\u0621\u064c \u0641\u064a\u0647\u0650 \u0625\u062f\u0627\u0645\u064c \u0623\u0648 \u0637\u0639\u0627\u0645\u064c \u0623\u0648 \u0634\u064e\u0631\u0627\u0628\u064c \u060c \u0641\u0625\u0630\u0627 \u0647\u064a\u064e \u0642\u062f \u0623\u064e\u062a\u064e\u062a\u0652\u0643\u064e \u060c \u0641\u0627\u0642\u0631\u064e\u0623 \u0639\u0644\u064e\u064a\u0647\u0627 \u0627\u0644\u0633\u0651\u064e\u0644\u0627\u0645\u064e \u0645\u0650\u0646 \u0631\u0628\u0651\u0650\u0647\u0627 \u0648 \u0645\u0650\u0646\u0651\u0650\u064a \u060c \u0648 \u0628\u0634\u0651\u0650\u0631\u0652\u0647\u0627 \u0628\u0628\u064e\u064a\u062a\u064d \u0641\u064a \u0627\u0644\u062c\u0646\u0651\u064e\u0629\u0650 \u0645\u0650\u0646 \u0642\u0635\u064e\u0628\u064d \u060c \u0644\u0627 \u0635\u064e\u062e\u0628\u064e \u0641\u064a\u0647\u0627 \u0648 \u0644\u0627 \u0646\u064e\u0635\u0628\u064e<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[ Ewe Mtume wa Allah huyu Khadija amekuja akiwa na chombo ambacho ndani yake mna kitoweo, au chakula au kinywaji, atakapokujia mtolee salamu kutoka kwa Mala Wake, na mbashirie kasri ya vito huko peponi, hamtakuwa na makelele ndani yake wala taabu yoyote ]<\/span> (2)<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\"><strong>Huzuni juu ya Huzuni:<\/strong> <\/span><\/p>\n<p>Matukio haya yenye uchungu yalimtokea Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) katika kipindi cha masiku machache, hisia za huzuni na machungu yakawa yametawala moyo wake Baada ya hapo havikuacha kumuandama vituko kutoka kwa jamaa zake, kwani wao walikuwa wanamfanyia jeuri. Baada ya kufariki kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Twalib<\/span> walianza maudhi na mateso, mambo hayo\u00a0 yalimzidishia huzuni juu ya huzuni kiasi cha kuwakatia tamaa.<\/p>\n<p>Aliamua kuondoka na kuelekea <span style=\"color: #ff6600;\">Twaif<\/span>, kwa matarajio kuwa watu wa huko wangeitikia wito wake au wangemuhifadhi na kumnusuru dhidi ya jamaa zake. Hakumpata <span style=\"color: #ff6600;\">Twaif<\/span> aliyekuwa tayari katika hayo; bali hali ilikuwa ni kinyume kabisa na matarajio yake, kero na maudhi ilikuwa ni kubwa sana kuliko ile aliyoipata kutoka kwa jamaa zake.<\/p>\n<p>Kama ambavyo uovu wa watu wa Makka ulivyozidi kwa Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) ndivyo ulivyozidi kwa Masahaba zake. Mpaka hatua ya kukimbia ra\ufb01ki yake <span style=\"color: #ff6600;\">Abubakar Al-Siddiq<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake). Kwa lengo la kuihama Makka, alitoka mpaka akafika mahali paitwapo Birak Al-Ghimad akiwa na makusudio ya kuelekea Ethiopia, <span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Ad-Daghna<\/span> ndiye aliyemrudisha katika dhamana yake.<\/p>\n<p><span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Ishaq<\/span> amesema kuwa, \u201dWakati alipofariki Abu Twalib, Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) na Masahaba zake walipata maudhi na mateso kutoka kwa Makuraishi ambayo hawakuwahi kuyapata wakati wa uhai wake. Inasemwa kuwa, siku moja mjinga mmoja, miongoni mwa wajinga wa Kikureishi, alimzuia na kumwagia Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) kichwani mwake mchanga. Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alirudi nyumbani kwake akiwa na mchanga kichwani mwake, mmoja kati ya mabinti zake alisimama akawa anauosha mchanga huo na huku akilia, wakati huo Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) akimliwaza kwa kumwambia:<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0644\u064e\u0627 \u062a\u064e\u0628\u0652\u0643\u0650\u064a \u064a\u064e\u0627 \u0628\u064f\u0646\u064e\u064a\u0651\u064e\u0629\u0650\u060c \u0641\u064e\u0625\u0650\u0646\u0651\u064e \u0627\u0644\u0644\u0651\u064e\u0647\u064e \u0645\u064e\u0627\u0646\u0650\u0639\u064c \u0623\u064e\u0628\u064e\u0627\u0643\u064e<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[ Usilie ewe binti yangu, hakika Mwenyezi Mungu\u00a0 Atamlinda baba yako.]<\/span><\/p>\n<p>Na akawa akimueleza kuwa kabla hapo:<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0645\u064e\u0627 \u0646\u064e\u0627\u0644\u064e\u062a\u0652 \u0645\u0650\u0646\u0651\u0650\u064a \u0642\u064f\u0631\u064e\u064a\u0652\u0634\u064c \u0634\u064e\u064a\u0652\u0626\u064b\u0627 \u0623\u064e\u0643\u0652\u0631\u064e\u0647\u064f\u0647\u064f\u060c \u062d\u064e\u062a\u0651\u064e\u0649 \u0645\u064e\u0627\u062a\u064e \u0623\u064e\u0628\u064f\u0648 \u0637\u064e\u0627\u0644\u0650\u0628\u064d<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\">[ Makuraishi hawakuthubutu kumfanyia kitu ambacho nikikichukia mpaka alipofariki Abu Twalib.] <span style=\"color: #000000;\">(3)<\/span><\/span><\/p>\n<p>Kwa sababu ya kuandamana kwa matukio yenye machungu katika mwaka huu, Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) aliuita mwaka huu, <strong>\u2019Mwaka wa huzuni&#8217;<\/strong> na kwa jina hili umekuwa unajulikana katika historia.<\/p>\n<p><strong><span style=\"color: #993300;\">Kumwoa Sauda (Radhi za Allah ziwe juu yake) <\/span><\/strong><\/p>\n<p>Mnamo mwezi wa Shawwal katika mwaka wa kumi wa Utume, Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alimwoa <span style=\"color: #ff6600;\">Sauda binti Zam&#8217;a<\/span>. Huyu alikuwa ni mmoja miongoni mwa Wale ambaio walisilimu zamani na kuhama katika ile Hijra ya pili kuelekea Uhabeshi, Mume wake alikuwa ni <span style=\"color: #ff6600;\">As-Sakran bin Amri,<\/span> aliyekuwa amesilimu na kuhama pamoja naye, akafariki Uhabeshi au baada ya kurejea Makka. Alipomaliza Eda yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alimposa na kumwoa. Huyu ndiye aliyekuwa mwanamke wa kwanza aliyemwoa baada ya kufariki kwa mke wake <span style=\"color: #ff6600;\">Khadija<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake), na baada ya miaka kadhaa kupita zamu yake alimpa Bibi\u00a0<span style=\"color: #ff6600;\">Aisha<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yao ).\u00a0 (4)<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1) Musnad Imam Ahmad Juzuu 6, Uk 118.<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>2) Sahihil Bulduri, Iuzuu 1, Uk. 539. <\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>3) Ibn Hisham, Juzuu 1, Uk. 416.<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>4) Rahmatun Lil \u2019Alamin, Iuzuu 2, Uk. 165. Talqiyh Fuhum Ahlul Athar, Uk. 10. 208 , Uk. 164. &#8211; .<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>*) Arrahiq Al-Makhtuum Uk 205-208<\/em><\/span><\/div>\n<hr \/>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Baada ya kufariki kwa Abu Twalib, kwa kiasi cha miezi miwili au mitatu (na hapa pana kauli mbili zinazotofautiana) alifariki dunia mama wa waumini Bi Khadija Al-Kubra (Radhi za Allah ziwe juu yake). Alifariki mnamo mwezi wa Ramadhani, mwaka wa kumi wa Utume, akiwa na umri wa miaka sitini na tano na Mtumbe [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-19212","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/19212","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=19212"}],"version-history":[{"count":3,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/19212\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":19306,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/19212\/revisions\/19306"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=19212"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=19212"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=19212"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}