{"id":17887,"date":"2022-11-10T11:53:31","date_gmt":"2022-11-10T11:53:31","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=17887"},"modified":"2023-01-26T08:20:35","modified_gmt":"2023-01-26T08:20:35","slug":"ujumbe-wa-mwisho-wa-makureish-kwa-abu-twalib","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/ujumbe-wa-mwisho-wa-makureish-kwa-abu-twalib\/","title":{"rendered":"UJUMBE WA MWISHO WA MAKUREISH KWA ABU TWALIB"},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alitoka pamoja na iliokuwa nao katika bonde, Shi\u2019ib Abu Twalib na akaendelea kufanya shughuli zake katika hali yake ya kawaida. nao pamoja na kuwa waliacha kuwatenga Banu Hashim, hawakuacha kuwakandamiza na kuwazuilia na njia ya Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfb<\/span>). Abu Twalib aliendelea kumkinga na uadui mtoto wa ndugu yake, lakini umri wake ulishakuwa ni mkubwa unaovuka miaka themanini, hali yake haikuwa nzuri na haswa baada ya miaka mitatu ya kutengwa, ilidhoofisha viungo vyake na kudhoofisha afya yake kwa ujumla. Haukupita muda ila maradhi yalimuandama. Wakati huo Mushirikina waliogopea sifa yao kuonekana ni mbaya kwa Waarabu, iwapo baada ya kufa kwake watafanya jambo lolote baya kwa mtoto wa ndugu yake. Kwa ajili hiyo wakafanya mbinu kwa mara nyingine tena kujadiliana na Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) mbele ya ammi yake Abu Twalib, na watoe baadhi ya yale ambayo hawakuwa radhi kuyatoa huko nyuma kumpa Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>), wakaamua kupeleka ujumbe na huo ulikuwa ndiyo ujumbe wao wa mwisho kwa Abu Twalib.<\/p>\n<p>Ibn Ishaq na wengine walisema: Abu Twalib alipopatwa na maradhi mazito, taarifa ziliwa\ufb01kia Makuraishi, walizungumza miongoni mwao na kusema kwa, \u2019Hakika Hamza na Umar wamesilimu na limekwisha tangaa jambo la Muhammad katika makabila ya Makuraishi wote. Kwa hiyo, twendeni kwa Abu Twalib tumuombe amzuie mtoto wa ndugu yake na amtoe kwetu, tunaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu hatutakubali atunyanganye jambo letu.\u201d Katika tamko jengine: \u201cHakika sisi tunaogopea kifo&#8217; cha mzee huyu, na kumtokea yatakayomtoea na Waarabu kupata ya kusema: \u2019Wamemwacha mpaka alipo kufa ammi yake ndipo walipomfanyia uovu \u201d<\/p>\n<p>Walikwenda kwa Abu Twalib, wakaongea naye na katika ujumbe ule walichaguliwa watu mashuhuri zaidi katika watukufu wa Kikuraishi na idadi yao ilikuwa ni ishiri na wa tano; miongoni mwao walikuwa ni: \u2018<span style=\"color: #ff6600;\">Utba bin Rabia,<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Shayba bin Rabia,<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Jahli bin Hisham,<\/span> <span style=\"color: #ff6600;\">Umayya bin Khalaf<\/span> na <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Sufyan bin Harb.<\/span> Wakasema kumwambia Abu Twalib: \u201cEwe Abu Twalib, wewe unafahamu nafasi yako kwetu, na wamehudhuria wanao, na tunahofia hali yako, na unalijua Iile ambalo liko baina yetu na mtoto wa ndugu yako. Kwa hiyo, mwite mchukulie kutoka kwetu na tumchukulie sisi kutoka kwake, ili ajizuie na sisi tujizuie naye na atuache sisi na dini yetu na tutamwacha yeye na Dini yake.\u201d<\/p>\n<p>Baada ya kupokea ujumbe wa Makuraishi, <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Twalib<\/span> alipeleka ujumbe kwa Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) na alipomjia akamwambia: \u201cEwe mtoto wa ndugu yangu, hawa ni mabwana katika jamaa zako wamekusanyika ili wakupe na wachukue kutoka kwako (mpate kukubaliana)\u201d, kisha akamweleza yale ambayo wamemweleza na waliyoyapendekeza kwak\u00e9, miongopi mwa hayo ni kuwa kila kundi lisipjgane na kundi lingine. Mtume _wa Mwenyezi Mungpi (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) akajibu kwa kuwaambia:<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0623\u0631\u064a\u062a\u0645 \u0625\u0646 \u0623\u0639\u0637\u064a\u062a\u0643\u0645 \u0643\u0644\u0645\u0629 \u062a\u0643\u0644\u0645\u062a \u0628\u0647\u0627 \u0648\u0645\u0644\u0643\u062a\u0645 \u0628\u0647\u0627 \u0627\u0644\u0639\u0631\u0628 \u0648\u062f\u0627\u0646\u062a \u0644\u0643\u0645 \u0627\u0644\u0639\u062c\u0645<\/span><\/p>\n<p><em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201cHivi mwaonaje kama nitawapa tamko moja tu ambalo mkulikubali mtameza kuwatawala _Waarabu wote na Waajemi kuwalipa nyie kodi?.\u201d <\/span><\/em><\/p>\n<p>Katika tamko lingine lililopokelewa ni kuwa alimwambia Abu Twalib; <span style=\"color: #0000ff;\">&#8220;Ninawataka watamke tamko moja tu wutakapolitamka, Waarabu wate watakuwa china yao nu kwa tamko hilo watatoa Waajemi kodi.\u201d<\/span> Katika tamko jingine alisema; <em><span style=\"color: #0000ff;\">&#8220;Ewe Ammi yangu kwa nini huwalitaki katika lile ambalo ni bora sana kwao?.&#8221;<\/span><\/em> Akauljza ammi yake; <em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201dUnawalingania kwenye jambo gani?.\u201d Mtume (\ufdfa) akasema; &#8220;Niwalingania kwenye kutamka neno moja tu ambalo kwa tamko hilo Waarabu wote watakuwa chini yao na watawamiliki kwalo Waajemi.&#8221;<\/span><\/em><\/p>\n<p>Kwa tamko la upokezi wa Ibn Is&#8217;haq\u00a0 <em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201cTamko maja tu ambalo mkilitoa mtawamiliki kwalo Waarabu nu Waajemi watakuwa china yenu.\u201d<\/span><\/em> Alipoyasema maneno hayo, walishangaa na wakatoshewa na hawakujua vipi watalikataa hili tamko moja lenye manufaa kwenye mpaka na kiwango hiki. Kisha Abu Jahli akasema, &#8220;Ni tamko gani hilo? Tunaapa kwa jina la baba yako, tupe tamko hilo na kumi mfano wake\u201d, akasema:<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">\u062a\u0642\u0648\u0644\u0648\u0646: \u0644\u0627\u0625\u0644\u0647 \u0625\u0644\u0627 \u0627\u0644\u0644\u0647 \u0648\u062a\u062e\u0644\u0639\u0648\u0646 \u0645\u0627 \u062a\u0639\u0628\u062f\u0648\u0646 \u0645\u0646 \u062f\u0648\u0646\u0647<\/span><\/p>\n<p>\u201cMtasema Hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfb<\/span>) na mviache vile mnavoviabudu kinyume na Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfb<\/span>).\u201d<\/p>\n<p>Wakapiga makofi, kisha wakasema: \u201dHivi unataka ewe Muhammad kuwafanya waungu wote kuwa Mungu mmoja tu? Hakika jambo lako linastaajabisha sana.\u201d<\/p>\n<p>Kisha baadhi yao wakasema: \u201dHakika mtu huyu hatotoa chochote kuwapa mnachotaka au kuwakubalia mnayoyataka, ondokeni na endeleeni na dini ya baba zenu mpaka atakapo hukumu Mwenyezi Mungu kati yenu na kati yake.\u201d Kisha wakatawanyika.<\/p>\n<p>Kuhusiana na watu hawa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfb<\/span>) Aliteremsha Maneno Yake:<\/p>\n<p style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0635\u0653\u06da \u0648\u064e\u0671\u0644\u06e1\u0642\u064f\u0631\u06e1\u0621\u064e\u0627\u0646\u0650 \u0630\u0650\u064a \u0671\u0644\u0630\u0651\u0650\u0643\u06e1\u0631\u0650 \u0628\u064e\u0644\u0650 \u0671\u0644\u0651\u064e\u0630\u0650\u064a\u0646\u064e \u0643\u064e\u0641\u064e\u0631\u064f\u0648\u0627\u0652 \u0641\u0650\u064a \u0639\u0650\u0632\u0651\u064e\u0629\u0656 \u0648\u064e\u0634\u0650\u0642\u064e\u0627\u0642\u0656 \u0643\u064e\u0645\u06e1 \u0623\u064e\u0647\u06e1\u0644\u064e\u0643\u06e1\u0646\u064e\u0627 \u0645\u0650\u0646 \u0642\u064e\u0628\u06e1\u0644\u0650\u0647\u0650\u0645 \u0645\u0651\u0650\u0646 \u0642\u064e\u0631\u06e1\u0646\u0656 \u0641\u064e\u0646\u064e\u0627\u062f\u064e\u0648\u0627\u0652 \u0648\u0651\u064e\u0644\u064e\u0627\u062a\u064e \u062d\u0650\u064a\u0646\u064e \u0645\u064e\u0646\u064e\u0627\u0635\u0656 \u0648\u064e\u0639\u064e\u062c\u0650\u0628\u064f\u0648\u0653\u0627\u0652 \u0623\u064e\u0646 \u062c\u064e\u0627\u0653\u0621\u064e\u0647\u064f\u0645 \u0645\u0651\u064f\u0646\u0630\u0650\u0631\u065e \u0645\u0651\u0650\u0646\u06e1\u0647\u064f\u0645\u06e1\u06d6 \u0648\u064e\u0642\u064e\u0627\u0644\u064e \u0671\u0644\u06e1\u0643\u064e\u0670\u0641\u0650\u0631\u064f\u0648\u0646\u064e \u0647\u064e\u0670\u0630\u064e\u0627 \u0633\u064e\u0670\u062d\u0650\u0631\u065e \u0643\u064e\u0630\u0651\u064e\u0627\u0628\u064c \u0623\u064e\u062c\u064e\u0639\u064e\u0644\u064e \u0671\u0644\u06e1\u0623\u0653\u0644\u0650\u0647\u064e\u0629\u064e \u0625\u0650\u0644\u064e\u0670\u0647\u0657\u0627 \u0648\u064e\u0670\u062d\u0650\u062f\u064b\u0627\u06d6 \u0625\u0650\u0646\u0651\u064e \u0647\u064e\u0670\u0630\u064e\u0627 \u0644\u064e\u0634\u064e\u064a\u06e1\u0621\u064c \u0639\u064f\u062c\u064e\u0627\u0628\u065e<\/span><br \/>\n<span style=\"color: #008000;\">\u0648\u064e\u0671\u0646\u0637\u064e\u0644\u064e\u0642\u064e \u0671\u0644\u06e1\u0645\u064e\u0644\u064e\u0623\u064f \u0645\u0650\u0646\u06e1\u0647\u064f\u0645\u06e1 \u0623\u064e\u0646\u0650 \u0671\u0645\u06e1\u0634\u064f\u0648\u0627\u0652 \u0648\u064e\u0671\u0635\u06e1\u0628\u0650\u0631\u064f\u0648\u0627\u0652 \u0639\u064e\u0644\u064e\u0649\u0670\u0653 \u0621\u064e\u0627\u0644\u0650\u0647\u064e\u062a\u0650\u0643\u064f\u0645\u06e1\u06d6 \u0625\u0650\u0646\u0651\u064e \u0647\u064e\u0670\u0630\u064e\u0627 \u0644\u064e\u0634\u064e\u064a\u06e1\u0621\u065e \u064a\u064f\u0631\u064e\u0627\u062f\u064f \u0645\u064e\u0627 \u0633\u064e\u0645\u0650\u0639\u06e1\u0646\u064e\u0627 \u0628\u0650\u0647\u064e\u0670\u0630\u064e\u0627 \u0641\u0650\u064a \u0671\u0644\u06e1\u0645\u0650\u0644\u0651\u064e\u0629\u0650 \u0671\u0644\u06e1\u0623\u0653\u062e\u0650\u0631\u064e\u0629\u0650 \u0625\u0650\u0646\u06e1 \u0647\u064e\u0670\u0630\u064e\u0627\u0653 \u0625\u0650\u0644\u0651\u064e\u0627 \u0671\u062e\u06e1\u062a\u0650\u0644\u064e\u0670\u0642\u064c<\/span><\/p>\n<p><em><span style=\"color: #0000ff;\">&#8220;S&#8217;ad, Naapa kwa Qur&#8217;ani yenye mawaidha Lakini walio kufuru wamo katika majivuno na upinzani Mataifa mangapi tumeyaangamiza kabla yao, na wakapiga kelele, lakini wakati wa kuokoka ulikwisha pita.Na walistaajabu kuwajia mwonyaji anaye tokana nao wenyewe, na makafiri wakasema: Huyu ni mchawi, mwongo.Amewafanya miungu wote kuwa ni Mungu Mmoja tu? Hakika hili ni jambo la ajabu. <span class=\"ttc\">Na wakaondoka wakubwa wao wakiwaambia: Nendeni zenu na dumuni na miungu yenu, kwani hili ni jambo lililo pangwa. <\/span><\/span><span style=\"color: #0000ff;\"><span class=\"ttc\">Sisi hatukusikia haya katika mila hii ya mwisho. Haya si chochote ila ni uzushi tu.<\/span> (38:1-6)<\/span><\/em><\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1) Ibnu Hishaam Juzaa 1, Uk 417-419<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>2) Tafhimul Qura&#8217;n Juzuu 4 Uk. 316-418, Mukhtasir sira Uk 91<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>3) Arrahiiq Al Makhtuum, Uk 199-202<\/em><\/span><\/div>\n<hr \/>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Mtume wa Mwenyezi Mungu (\ufdfa) alitoka pamoja na iliokuwa nao katika bonde, Shi\u2019ib Abu Twalib na akaendelea kufanya shughuli zake katika hali yake ya kawaida. nao pamoja na kuwa waliacha kuwatenga Banu Hashim, hawakuacha kuwakandamiza na kuwazuilia na njia ya Mwenyezi Mungu (\ufdfb). Abu Twalib aliendelea kumkinga na uadui mtoto wa ndugu yake, [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-17887","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/17887","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=17887"}],"version-history":[{"count":5,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/17887\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":19207,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/17887\/revisions\/19207"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=17887"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=17887"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=17887"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}