{"id":17580,"date":"2022-11-08T12:27:09","date_gmt":"2022-11-08T12:27:09","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=17580"},"modified":"2022-11-10T10:25:03","modified_gmt":"2022-11-10T10:25:03","slug":"kubatilika-kwa-mkataba","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/kubatilika-kwa-mkataba\/","title":{"rendered":"KUBATILIKA KWA MKATABA"},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #993300;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Mambo yaliendelea namna hii kwa muda wa miaka mitatu kamili. Katika mwezi wa Muharram, 2 ikiwa ni mwaka wa kumi wa Utume, ilikuwa ndiyo siku ya kubatilishwa kwa mkataba na kuvunjika. Kwa sababu ya tofau\ufb01 zilizozuka kati ya Makuraishi, maana kutokea mwanzo, wapo waliounga mkono mkataba huo na wapo walioupinga. Wale waliokuwa wanapinga mkataba huo walikuwa wakiongozwa na <span style=\"color: #ff6600;\">Hisham bin \u2019Amru<\/span> kutoka katika kabila la Banu Amir bin Luay aliyekuwa akiwaendea Banu Hashim katika bonde kwa kuji\ufb01cha wakati wa usiku akiwapelekea chakula, (maana yeye alikwishawahi kumuendea <span style=\"color: #ff6600;\">Zuhair bin Abi Umayya al-Makhzoumy<\/span> na ambaye mama yake alikuwa ni <span style=\"color: #ff6600;\">\u2018Aatikah binti Abdil-Mutwalib),<\/span> na kumuuliza, \u201cEwe Zuhair hivi ni kweli kuwa umeridhia kula chakula na kunywa maji na hali ya kuwa wajomba zako wamo ka\ufb01ka hali ambayo unaijua?\u201d Naye akajibu: \u201dRehema iwe juu yako, nitafanya nini wakati mimi ni mtu mmoja tu? Ama, Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu, laiti kungelikuwa na mtu mwingine aliye tayari, mimi ningekuwa wa kwanza kuubatilisha mkataba huu\u201d, hapo Hisham akamwambia basi kwa hakika sasa umempata mtu uliyekuwa unamtaka, baada ya hapo wakakubaliana kuwa watafute na mtu wa tatu. 1<\/p>\n<p>Akaenda kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Mut\u2019im bin \u2019Adiy,<\/span> akamkumbusha udugu wa Banu Hashim na Banu Al-Mutwalib watoto wa Abdi Manafi akamlaumu juu ya kuwaunga mkono Makuraishi kwa dhulma hii, <span style=\"color: #ff6600;\">Mut\u2019im bin \u2018Adiy<\/span> akasema: \u201dRehema iwe juu yako, nitafanya nini? Kwa hakika si vinginevyo, ni mtu mmoja tu\u201d, Akaambiwa \u201cUmempata na mtu wa pili\u201d, akauiiza, \u201cNani huyo?\u201d Akajibiwa, \u201cNi mimi\u201d; Mut\u2019im akasema, \u201cNipatie mtu wa tatu\u201d, _ Akajibiwa, \u201cNimekwishafanya hivyo\u201d; Akauliza tena, \u201cNi nani huyo mtu wa tatu?\u201d Akaelezwa, \u201cNi <span style=\"color: #ff6600;\">Zuhair bin Abu Umayya<\/span>.\u201d Wakakubaliana kuwa watafute na mtu wa nne, akaenda kwa A<span style=\"color: #ff6600;\">bu Al-B\u2019ulahtari bin Hisham,<\/span> akamweleza mfano wa yale aliyomweleza Mut\u2019im. Akaulizwa, \u201dJe, kuna mtu yeyote ambaye atasaidia katika hili?\u201d Akajibiwa; \u201dNdiyo.\u201d Akauliza; \u201cNi nani huyo?\u201d Akajibiwa; \u201cNi <span style=\"color: #ff6600;\">Zuhair bin Abu Umayya<\/span> na <span style=\"color: #ff6600;\">Mut\u2019im bin \u201cAdiy,<\/span> na mimi niko pamoja nawe.\u201d Wakakubaliana kuwa watafute na mtu wa tano, akamwendea <span style=\"color: #ff6600;\">Zamgha bin Al-Aswad bin Ali-Mutwalib bin -Assad,<\/span> akazungumza naye, akamkubusha juu ya udugu wao na haki yao, akaulizwa, \u201dJe, yuko mtu yeyote mwingine ka\ufb01ka hili jambo unailoniitia?\u201d Akajibiwa, \u201dNdiyo.\u201d Siku waliyo kubaliana ilipo\ufb01ka wakakutanika mahali paitwapo _<span style=\"color: #ff6600;\">Al- Hajouni,<\/span> wakakubaliana kuubalilisha ule mkataba, Zuhair akasema: \u201cMimi nitakuwa mtu wa kwanza kuzungumza.\u201d<\/p>\n<p>Asubuhi ya siku ya pili kama ilivyokuwa kawaida yao walikwenda kwenye mabaraza yao, asubuhi hiyo Zuhair alikwenda akiwa katika vazi maalumu. Aliizunguka Al- Ka\u2019aba mara saba, kisha akawaelekea watu waliokuwepo. Akasema, \u201dEnyi watu wa Makka, hivi tunaona fakhari gani kula chakula na kuvaa nguo wakati Banu Hashim wanaangamia? Hawauziwi kitu na hapanunuliwi kutoka kwao? Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu, sitakaa chini mpaka upasuliwe ubao ulioandikwa mkataba huu ulio na dhulma na unaokata udugu.\u201d<\/p>\n<p>Abu Jahli aliyekuwa katika upande wa Msikiti alisimama na kusema, \u201dUmesema uwongo, Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu kibao (ulioandikwa ule rnkataba) hakitapasuliwa.\u201d Hapo <span style=\"color: #ff6600;\">Zam\u2019a Bin Al-Aswad<\/span> naye akasimama na kusema: \u201cNinaapa kwa Jina la Mwenyezi Mungu, wewe ni mwongo zaidi, si wote tulioridhia wakati wa kuandikwa kwake. <span style=\"color: #ff6600;\">Abu Al-Bukhtari<\/span> alisimama na kuunga mkono; \u201dAmesema kweli Zam\u2019a, hatuyaridhii yale ambayo yameimdikwa, na hatuyakubali\u201d, na hapo akasimarna <span style=\"color: #ff6600;\">Mut\u2019im bin \u2019Adiy<\/span> na kusema: \u201cMmesema kweli na amesema uwongo yule ambaye amesema kinyurne na hayo, tunajiepusha kwa Mwenyezi Mungu na kibao hicho na yaliyomo ndani yake.\u201d <span style=\"color: #ff6600;\">Hisham bin Amity<\/span> nae akaunga mkono hoja kwa kusema maneno mfano wa hayo. Abu Jahli akasema, \u2019Hili ni jambo lililoamuliwa usiku, mahali pengine pasipokuwa hapa.\u2019 \u2013 Wakati maneno hayo yakisemwa Abu Twalib alikuwa amekaa upande wa msikiti, na ali\ufb01ka pale kwani alishajua kuwa Wahyi umeteremshiwa kwa mtoto wa nduguye kuwa: \u2018Mchwa wameshautafuna ule mkataba, isipokuwa kilichobakia ni Jina la Allah <span style=\"color: #008000;\">(\ufdfb)<\/span> lililokuwa ndani ya maandishi yale.\u201d Abu Twalib aliwakabili Makuraishi na kuwaeleza, \u201dMtoto wa ndugu yangu amenieleza kadha na kadha\u2026.. (na akawaeleza kibao kuliwa na mchwa); Niko tayari kuwapa Muhammad (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) mumfanye mtakavyo yakiwa maneno aliyoyasema sio sahihi, au muendelee na kuwatenga kama ilivokuwa kwa muda wa miaka mitatu iliyopita. Watu wote wa Makka walikubaliana na pendekezo lake. Wakasema umefanya uadilifu, na baada ya mazungiunzo kati yao na Abu Jahl. Mut\u2019im alikwenda ili aubandue ule mkataba, alitaharuki kwa kukuta kuwa wote umeshaliwa na mchwa isipokuwa pale palipoandikwa, \u201dKwa Iina Lako Ewe Mela.\u201d<\/p>\n<p>Ubatilishaji wa mktaba ulikamilika na Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alitoka katika bonde, Ash-Shib, na waliokuwa pamoja naye. Mushirikinaa wakawa wameonyeshwa daljli kubwa miongoni mwa dalili za Utume wake, isipokuwa kama alivyokwisha kueleza Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfb<\/span>) kuhusiana nao:<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0648\u064e\u0625\u0650\u0646 \u064a\u064e\u0631\u064e\u0648\u06e1\u0627\u0652 \u0621\u064e\u0627\u064a\u064e\u0629\u0657 \u064a\u064f\u0639\u06e1\u0631\u0650\u0636\u064f\u0648\u0627\u0652 \u0648\u064e\u064a\u064e\u0642\u064f\u0648\u0644\u064f\u0648\u0627\u0652 \u0633\u0650\u062d\u06e1\u0631\u065e \u0645\u0651\u064f\u0633\u06e1\u062a\u064e\u0645\u0650\u0631\u0651\u065e<\/span><\/p>\n<p><em><span style=\"color: #0000ff;\">\u201cNa wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea.\u201d (54:2)<\/span> <\/em><\/p>\n<p>Hawakuijali dalili hiyo na wakauongeza uka\ufb01ri juu ya ukafiri wao.<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>3) Arrahiiq Al Makhtuum, Uk 184-189<\/em><\/span><\/div>\n<hr \/>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Mambo yaliendelea namna hii kwa muda wa miaka mitatu kamili. Katika mwezi wa Muharram, 2 ikiwa ni mwaka wa kumi wa Utume, ilikuwa ndiyo siku ya kubatilishwa kwa mkataba na kuvunjika. Kwa sababu ya tofau\ufb01 zilizozuka kati ya Makuraishi, maana kutokea mwanzo, wapo waliounga mkono mkataba huo na wapo walioupinga. Wale waliokuwa wanapinga [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-17580","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/17580","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=17580"}],"version-history":[{"count":5,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/17580\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":17886,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/17580\/revisions\/17886"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=17580"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=17580"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=17580"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}