{"id":17569,"date":"2022-11-08T09:14:34","date_gmt":"2022-11-08T09:14:34","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=17569"},"modified":"2022-11-08T09:14:37","modified_gmt":"2022-11-08T09:14:37","slug":"ususiaji-wa-kijamii-kwa-ujumla","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/ususiaji-wa-kijamii-kwa-ujumla\/","title":{"rendered":"USUSIAJI WA KIJAMII KWA UJUMLA"},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Katika kipindi Cha majuma manne yalitokea matukio makubwa manne upande wa Mushirikina. Kwanza, katika muda huo mchache alisilimu Hamza; Pili, akasilimu Umar; Tatu, Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alikataa makubaliano nao; Nne, mkataba wa pamoja baina ya Banu Al-Mutwalib na Banu Hashim wa kumlinda na kumhami Mtume <span style=\"color: #008000;\">(\ufdfa<\/span>). Mambo yote haya yaliwachanganya Mushirikina na walifahamu kuwa lau wakiamua kumwua Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) basi Makka nzima ingemwagika damu na huenda kwa hilo wangemalizika. Kwa utambuzi huo wa mambo wakabadilisha mikak&#8217;ati yao na kuelekea kwenye dhulma ya chini zaidi kuliko kuua.<\/p>\n<p><span style=\"color: #993300;\">AHADI YA DHULMA NA UADUI<\/span><\/p>\n<p>Katika kuendeleza njama zao dhidi ya Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) Makuraishi walikusanyika katika sehemu iitwayo Wadi AI- Muhassab sehemu iliyokuwa chini ya milki ya Banu Kinana Khaifu ya Banu Kinana (Khaifu-ni sehemu ambayo imeporomoka katika kitako cha jabali kisha ikanyanyuka na kuwa mbali ya mapito ya maji katika jangwa la Al-Muhassab). Hapo walipeana kiapo cha kusaidiana dhidi ya Banu Hashim na Banu Al-Mutwalib kuwa: Wasioleane nao, wasifanye biashara nao, wasichanganyikane nao, na wasiseme nao mpaka watakapo mkabidhi kwao Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) kwa ajili ya kumwua; Makubaliano hayo yaliandikwa katika waraka ambao ndani yake waliweka mkataba huo wa ahadi_ wadhulma na uadui, ambamo miongoni mwa masharti yake yalikuwa ni: Wasikubali kutoka kwa Banu Hashim suluhu ya aina yoyote milele, na wasiwe na huruma yoyote na watu wa kabila la Banu Hashim mpaka hapo watakapomkabidhi Mtume (\ufdfa) kwao ili wamuue.<\/p>\n<p>Ibnul Qayyim, anasema, inasemekana kibao cha waraka huo kiliandikwa na <span style=\"color: #ff6600;\">Mansour bin Ikrima bin Amir bin Hashim bin al-Harith,<\/span> lakini kwa usahihi zaidi ni <span style=\"color: #ff6600;\">Baghiidh bin Amir bin Hashim,<\/span> ambaye Mtumc (\ufdfa) alimuapiza na hivyo kupooza mkono wake.<\/p>\n<p>Baada ya mkataba huo kukamilika, kibao kilitundikwa ndani ya Al-Ka\u2019aba, Banu Hashim na Banu Al-Mutwalib wakatengwa wote, wakiwemo Waislamu na maka\ufb01ri katika koo hizo, isipokuwa Abu-Lahb, wakazuiwa katika bonde la Abu Twalib, mwanzo mwa mwezi Muharram, Mwaka wa saba mpaka wa kumi toka kupewa utume, yaani kipindi cha miaka Mitatu.<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1) Arrahiiq Al Makhtuum, Uk 192-193<\/em><\/span><\/div>\n<hr \/>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Katika kipindi Cha majuma manne yalitokea matukio makubwa manne upande wa Mushirikina. Kwanza, katika muda huo mchache alisilimu Hamza; Pili, akasilimu Umar; Tatu, Mtume (\ufdfa) alikataa makubaliano nao; Nne, mkataba wa pamoja baina ya Banu Al-Mutwalib na Banu Hashim wa kumlinda na kumhami Mtume (\ufdfa). Mambo yote haya yaliwachanganya Mushirikina na walifahamu kuwa [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-17569","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/17569","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=17569"}],"version-history":[{"count":2,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/17569\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":17571,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/17569\/revisions\/17571"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=17569"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=17569"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=17569"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}