{"id":17556,"date":"2022-11-08T07:19:09","date_gmt":"2022-11-08T07:19:09","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=17556"},"modified":"2022-11-08T07:35:15","modified_gmt":"2022-11-08T07:35:15","slug":"mwakilishi-wa-makuraish-kwa-mtume-%ef%b7%ba","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/mwakilishi-wa-makuraish-kwa-mtume-%ef%b7%ba\/","title":{"rendered":"MWAKILISHI WA MAKURAISH KWA MTUME \ufdfa"},"content":{"rendered":"<hr \/>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr \/>\n<p>Baada ya kusilimu hawa mashujaa wawili watukufu, Hamza bin Abdil Mutwalib na \u2018Umar bin al-Khattab (Radhi za Allah ziwe juu yao), mawingu ya udhalimu na mateso dhidi ya Waislamu yalianza\u00a0 kutanzuka na Mushirikina wa Makka walianza kuona kuwa hakuna maana tena ya kuendelea kuwatesa Waislamu. Washirikina wakaanza kubadilisha mbinu za mapambano na kuanza kujadiliana na Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) kwa kupinga hoja zake. jambo ambalo lilikuwa gumu nmo kwao. Yote haya waliyafanya kwa lengo la kutaka kumzuia kufanya kazi ya Da&#8217;awa na ku\ufb01kisha ujumbe aliotumwa Mwenyezi Mumgu {<span style=\"color: #008000;\">\ufdfb<\/span>).<\/p>\n<p>Kwa ujinga wao, hawakuwa wakifahamu maskini kuwa walikuwa wakishindana na mtu ambaye kamwe wasingeweza kumshinda, na kuwa Alichokikusudia Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfb<\/span>) ndicho kitakachokuwa. Hata baada ya juhudi zote walizofanya hawakuweza kufanikiwa na hawakuambulia kitu. Wakashindwa katika lile ambalo walikuwa wamelikusudia.<\/p>\n<p>Ibnu Is&#8217;haq alisema kuwa, alipokea kutoka kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Yazidi bin Ziadi<\/span> aliyepokea kutoka kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Muhammad bin Kaab Al- Quradhy,<\/span> alisema; \u201dNimeelezwa kuwa \u2019Utbah bin Rabia (miongoni mwa watukufu wa Kikuraish), alisemaz \u201dSiku moja wakati akiwa ka\ufb01ka Jumba la mikutano la Makuraishi, na Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) akiwa amekaa msikitini peke yake, alisema: \u201dEnyi jamaa miongoni mwa Makuraishi!, hivi sisi tunashindwa kweli kupata njia ya kumdhibiti Muhammad na haraka\ufb01 zake? Enyi Makuraishi! mnaonaje kama nikimuendea Muhammad na kuzungumza nae na kujaribu kumpendekezea mambo kadhaa ambayo natumai kuwa atayaridhia baadhi yake na kumuahidi kumpa chochote akitakacho ili mradi aache kuhubiri khabari za Mungu wake?.\u201d<\/p>\n<p>Jambo hili lilifanyika wakati aliposilimu Hamza (Radhi za Allah ziwe juu yake) na Mushirikina kuona kuwa Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) wanazidi kuongezeka idadi yao na kuwa wengi. Wakasema; \u201dBila shaka <span style=\"color: #ff6600;\">Abul Wahid,<\/span> nenda uzungmze nae.&#8221; Hapo ndipo \u2019Utbah aliposimama na kwenda mpaka alipom\ufb01kia Mtumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) na kusema: \u201cEwe mtoto wa ndugu yangu, kwa hakika wewe unajua daraja kubwa na cheo ulichonacho miongoni mwetu kwa uzao wako na nasabu yako. Kwa hakika umewaletea jamaa zako jambo kubwa sana, na kwa jambo hilo umeutenganisha mkusanyiko wao. Umedharau mwendo wao wa \ufb01kra na umeharibu ndoto zao. Umeaibisha kwa jambo hili miungu yao, dini yao, na kwa jambo lako hili umewakufurisha pia waliopita katika baba zao. Nisikilize, nitawasilisha kwako mapendekezo ambayo ninataka uyachunguze, na huenda ndani yake ukakubali baadhi yake.\u201d Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) akasema, <span style=\"color: #0000ff;\">\u201dSema ewe Abdul-Walid, ninakusikiliza&#8221;<\/span> akasema: \u201cEwe mtoto wa ndugu yangu, kwa hakika hakuna jambo jingine isipokuwa utueleze kuhusu hili ulilokuja nalo, kama unataka &#8216;Mali ili uliache tutakukusanyia mali zetu &#8216;na kukufanya kuwa tajiri kuliko mtu yeyote miongoni mwetu, na kama kwa jambo hili unataka utukufu basi tutakufanya Bwana wetu kiasi cha kutopitisha uamuzi wowote bila ya idhini yako, na ikiwa unataka utawala tutakufanya uwe Mfalme wetu, na kama hili linalokujia ni jini unaloliona na huwezi kulifukuza likawa mbali na nafsi yako tutakutafutia mganga na sisi tutatoa mali zetu katika jambo hili mpaka tukuponye.&#8221;<\/p>\n<p>Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alimsikiliza \u2019Utbah kwa makini mpaka alipomaliza, na kisha akamuuliza, <span style=\"color: #0000ff;\">\u201dUmemaIiza ewe Abul-Walid?&#8221;<\/span> Naye akajibu: ndiyo.\u00a0 Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) akaanza kusoma<\/p>\n<p style=\"text-align: right;\"><span style=\"color: #008000;\">\u062d\u0645\u0653 (1) \u062a\u064e\u0646\u0632\u0650\u064a\u0644\u065e \u0645\u0651\u0650\u0646\u064e \u0671\u0644\u0631\u0651\u064e\u062d\u06e1\u0645\u064e\u0670\u0646\u0650 \u0671\u0644\u0631\u0651\u064e\u062d\u0650\u064a\u0645\u0650 (2) \u0643\u0650\u062a\u064e\u0670\u0628\u065e \u0641\u064f\u0635\u0651\u0650\u0644\u064e\u062a\u06e1 \u0621\u064e\u0627\u064a\u064e\u0670\u062a\u064f\u0647\u064f\u06e5 \u0642\u064f\u0631\u06e1\u0621\u064e\u0627\u0646\u064b\u0627 \u0639\u064e\u0631\u064e\u0628\u0650\u064a\u0651\u0657\u0627 \u0644\u0651\u0650\u0642\u064e\u0648\u06e1\u0645\u0656 \u064a\u064e\u0639\u06e1\u0644\u064e\u0645\u064f\u0648\u0646\u064e (3) \u0628\u064e\u0634\u0650\u064a\u0631\u0657\u0627 \u0648\u064e\u0646\u064e\u0630\u0650\u064a\u0631\u0657\u0627 \u0641\u064e\u0623\u064e\u0639\u06e1\u0631\u064e\u0636\u064e \u0623\u064e\u0643\u06e1\u062b\u064e\u0631\u064f\u0647\u064f\u0645\u06e1 \u0641\u064e\u0647\u064f\u0645\u06e1 \u0644\u064e\u0627 \u064a\u064e\u0633\u06e1\u0645\u064e\u0639\u064f\u0648\u0646\u064e (4) \u0648\u064e\u0642\u064e\u0627\u0644\u064f\u0648\u0627\u0652 \u0642\u064f\u0644\u064f\u0648\u0628\u064f\u0646\u064e\u0627 \u0641\u0650\u064a\u0653 \u0623\u064e\u0643\u0650\u0646\u0651\u064e\u0629\u0656 \u0645\u0651\u0650\u0645\u0651\u064e\u0627 \u062a\u064e\u062f\u06e1\u0639\u064f\u0648\u0646\u064e\u0627\u0653 \u0625\u0650\u0644\u064e\u064a\u06e1\u0647\u0650 \u0648\u064e\u0641\u0650\u064a\u0653 \u0621\u064e\u0627\u0630\u064e\u0627\u0646\u0650\u0646\u064e\u0627 \u0648\u064e\u0642\u06e1\u0631\u065e \u0648\u064e\u0645\u0650\u0646\u06e2 \u0628\u064e\u064a\u06e1\u0646\u0650\u0646\u064e\u0627 \u0648\u064e\u0628\u064e\u064a\u06e1\u0646\u0650\u0643\u064e \u062d\u0650\u062c\u064e\u0627\u0628\u065e \u0641\u064e\u0671\u0639\u06e1\u0645\u064e\u0644\u06e1 \u0625\u0650\u0646\u0651\u064e\u0646\u064e\u0627 \u0639\u064e\u0670\u0645\u0650\u0644\u064f\u0648\u0646\u064e (5)<\/span><\/p>\n<p><span style=\"color: #0000ff;\"><em>Bismillahir Rahmanir Rahiim \u201d Han Mym. Uteremsho huu umetoka kwa Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu Hichi ni Kitabu kilicho pambanuliwa Aya zake, cha kusomwa kwa Kiarabu kwa watu wanao jua.Kitoacho khabari njema, na chenye kuonya. Lakini wengi katika wao wamepuuza; kwa hivyo hawasikii.Na wakasema: Nyoyo zetu zimo katika vifuniko kwa hayo unayo tuitia, na masikio yetu yana uziwi, na baina yetu na wewe lipo pazia. Basi wewe tenda, nasi tunatenda. \u201d<\/em>\u00a0<\/span> \u00a0(41:1-5)<\/p>\n<p>Mtume ((<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) aliendelea kumsomea kutoka Sura hiyo, \u2019Utbah Alinyamaza na kusikiliza kwa makini ilhali mikono yake ameiweka nyuma akiwa ameegemea. Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) aliendelea mpaka katika aya iliyohimiza sijida, akasujudu kisha akamwabia&#8217; Utbah, <span style=\"color: #0000ff;\">&#8220;Umeyasikia majibu yangu hivyo una\u00a0 hiari; kufanya utakalo,\u201d<\/span> \u2019Utbah alisimama kurudi kwa wenzak\u00e9.<\/p>\n<p>Walipomuona jinsi alivyosawajika, baadhi yao waliwaambia wenzi wao tunaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfb<\/span>), kwa hakika Abul-Waljd anawajieni katika hali sio ile aliyoondoka nayo. Aipofika walimuhoji kwa kumuuliza, Ni jambo gani lililokusibu Ewe Abul-Wa.lid?\u00a0 Naye akawajibu kwa kusema; \u201cMimi nimesikia maneno ambayo Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfb<\/span>) sijawahi kusikia mfano wake kabla ya leo. Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfb<\/span>), maneno hayo siyo mashairi, wala siyo uchawi na wala si maneno ya kuhani. Enyi jamaa zangu Makuraishil, ninakuombeni acheni hayo na mwacheni na mambo yake na jivueni nae. Kwa hiyo kaeni mbali naye. Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfb<\/span>), kwa hakika maneno ambayo nimeyasikia leo kwake yatakuwa na khabari kubwa sana iwapo Waarabu watamsikia na ikitokea kuwa watamdhuru hivyo itakuwa mumetoshelezwa na watu wengine. Lakini (Muhammad) akiwashinda Waarabu, ufalme wake utakuwa ni ufalme wenu na utukufu wake utakuwa ni utukufu wenu, na mtakuwa watu miongoni mwa watu walio na mafanikio makubwa kuliko watu wengine kwa sababu Yake. &#8221;<\/p>\n<p>Baada ya Makuraishi kumsikiliza Mjumbe wao, wakamwambia, \u201dAmekuroga!. Tunaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu, Ewe Abul-Walidl huyu amekuroga kwa ulimi wake\u201d, naye akawajibu; \u201cHaya ndiyo maoni yangu kwake kwa hivyo fanyeni lile ambalo mnaona linafaa. (1)<\/p>\n<p>Katika mapokezi mengine inaelezwa kuwa \u2018Utbah, aliendelea kusikiliza aya&#8217; za Qur&#8217;ani ambazo Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) alikuwa akisoma mpaka alipo\ufb01kia kwenye Kauli Yake Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfb<\/span>) Aliye Mtukufu:<\/p>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"color: #008000;\">\u0641\u064e\u0625\u0650\u0646\u06e1 \u0623\u064e\u0639\u06e1\u0631\u064e\u0636\u064f\u0648\u0627\u0652 \u0641\u064e\u0642\u064f\u0644\u06e1 \u0623\u064e\u0646\u0630\u064e\u0631\u06e1\u062a\u064f\u0643\u064f\u0645\u06e1 \u0635\u064e\u0670\u0639\u0650\u0642\u064e\u0629\u0657 \u0645\u0651\u0650\u062b\u06e1\u0644\u064e \u0635\u064e\u0670\u0639\u0650\u0642\u064e\u0629\u0650 \u0639\u064e\u0627\u062f\u0656 \u0648\u064e\u062b\u064e\u0645\u064f\u0648\u062f\u064e (13)<\/span><\/p>\n<p>\u00a0<em><span style=\"color: #0000ff;\">&#8220;Basi wakipuuza wewe sema: Nakuhadharisheni adhabu mfano wa adhabu ya A&#8217;di na Thamudi,\u201d<\/span><\/em> (41:13) &#8216;Utbah akasimama hali ya kuwa ni mwenye kufadhaika na akauweka mkono wake juu ya mdomo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) huku akisema, \u201cNinakuomba kwa jina la Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfb<\/span>) na kwa udugu na hilo ni kwa kuogopa kutoka katika lile ambalo limetahadharishwa (wasije wakangamia Makuraishi).&#8221; Akarudi kwa watu waliomtuma na akasema yale aliyoyasema. (2)<\/p>\n<div>\n<hr \/>\n<\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1) Ibnu Hishaam Juzaa 1, Uk 293-294<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>2) Tafsiri ibn Kathir Juzuu 6 Uk. 159-160-161,<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>3) Arrahiiq Al Makhtuum, Uk 184-189<\/em><\/span><\/div>\n<hr \/>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM Baada ya kusilimu hawa mashujaa wawili watukufu, Hamza bin Abdil Mutwalib na \u2018Umar bin al-Khattab (Radhi za Allah ziwe juu yao), mawingu ya udhalimu na mateso dhidi ya Waislamu yalianza\u00a0 kutanzuka na Mushirikina wa Makka walianza kuona kuwa hakuna maana tena ya kuendelea kuwatesa Waislamu. Washirikina wakaanza kubadilisha mbinu za mapambano na kuanza [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-17556","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/17556","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=17556"}],"version-history":[{"count":6,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/17556\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":17563,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/17556\/revisions\/17563"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=17556"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=17556"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=17556"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}