{"id":16891,"date":"2022-10-23T09:25:13","date_gmt":"2022-10-23T09:25:13","guid":{"rendered":"https:\/\/uongofu.com\/?p=16891"},"modified":"2022-11-08T08:48:59","modified_gmt":"2022-11-08T08:48:59","slug":"baada-ya-kusilimu-kwa-umar-bin-al-khattab-radhi-za-allah-ziwe-juu-yake","status":"publish","type":"post","link":"https:\/\/uongofu.com\/en\/baada-ya-kusilimu-kwa-umar-bin-al-khattab-radhi-za-allah-ziwe-juu-yake\/","title":{"rendered":"BAADA YA KUSILIMU KWA UMAR BIN AL-KHATTAB (Radhi za Allah ziwe juu yake)"},"content":{"rendered":"<hr>\n<p style=\"text-align: center;\"><span style=\"font-size: 18pt; color: #ff6600;\">AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM<\/span><\/p>\n<hr>\n<p class=\"aya_text\" style=\"text-align: left;\"><span style=\"color: #ff6600;\">&#8216;Umar bin Al-Khattab<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa ni mtu mwenye kuhieshimika mno na asiyechezewa, kwa hakika kusiliimu kwake kuliibua vurugu na kuwagonganisha Mushirikina na kuwafanya kuwa ni wanyonge na dhalili. Kukawavika Waislarnu nguvu, utukufu na furaha.<\/p>\n<p class=\"aya_text\" style=\"text-align: left;\">Ibn Ishaq amepokea kutoka kwa <span style=\"color: #ff6600;\">&#8220;Umar<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa; \u201dWakati niliposilimu nili\ufb01kiria ni nani katika watu wa Makka aliyekuwa na uadui mkubwa zaidi kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) nikakumbuka kuwa ni Abu Jahl, nilikwenda nyumbani kwake na kumgongea mlango, baada ya kufungua mlango na kunikaribisha aliniuliza; &#8220;Ni jambo gani ambalo limekuleta?\u201d Nikamjibu kuwa nimekwenda kumueleza kuwa sasa nim\u00e9kwisha kumwamini Mwenyezi Mungu (\ufdfb) na Mjumbe wake Muhammad (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>), na nimeyakubali yale ambayo amekuja nayo. Baada ya maneno hayo, Abu Iahal aliubamiza mlango usoni mwangu na kuniapiza, \u201dMwenyezi Mungu akuchukie na ayachukie mabaya yote uliyokuja nayo. (1)<\/p>\n<p class=\"aya_text\" style=\"text-align: left;\">Ibni Al-Jawzy alisema vile vile kuwa \u2018Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisema baada ya kusilimu kwake, kuwa ilikuwa ni kawaida ya Makuraishi kuwa mtu anapoingia katika Uislamu walimvaa na kupigana , lakini wakati niliposilimu (Umar) nilikwenda kwa mjomba wangu, <span style=\"color: #ff6600;\">Al-\u2018As bin Hashim<\/span> nikamfahamisha kusilimu kwangu (hakusema kitu) akaingia ndani. \u2019Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) anaendelea kusema kuwa: &#8216;Nikaenda kwa mtu miongoni mwa wakubwa wa Kikuraishi (Abu jahl) nae nilipomfahamisha pia akaingia ndani.\u2019 (2)<\/p>\n<p class=\"aya_text\" style=\"text-align: left;\"><span style=\"color: #ff6600;\">Ibni Hisham na Ibn Al-]awzy<\/span> nao pia kwa ufupi wametaja kuwa \u2018Umar aliposilimu alikwenda kwa Jamil bin Mu&#8217;ammar Al-Jumahy, aliyekuwa mzungumzaji mzuri miongoni mwa Makuraishi na kumueleza kuwa yeye amesilimu. Kwa sauti ya juu kabisa (huyu Jamil) akatoa ulingano kuwa Ibn Al-Khattab ametoka katika dini. &#8220;Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) aliyekuwa nyuma yake wakati huo alimkanusha kwa vile alisema uongo, na kusema yeye ameingia katika Uislamu, Makuraishi wakahamaki na kuanza kupigana nae, walipigana kwa kipindi kirefu mpaka \u2018Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) akaelemewa na kukaa chini. Wakasimama na kumzunguka na yeye akawaambia: &#8220;\u2019Panyeni mtakalo fanya, Ninaapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu (\ufdfb) laiti tungelikuwa watu mia tatu, tungewaacheni nyinyi au mngetuachia sisi.\u201d (3) Baada ya hapo Mushirikina walimtafuta nyumbani kwake wakikusudia kumwua.<\/p>\n<p class=\"aya_text\" style=\"text-align: left;\">Bukhari amepokea kutoka kwa Abdillah bin \u2019Umar, kuwa alisema: &#8220;Wakati Umar akiwa yumo nyumbani kwake amejaa khofu, gha\ufb02a alimjia <span style=\"color: #ff6600;\">Al-\u2019As bin Waili Al-Sahmy<\/span> (Abu Amru) akiwa na nguo mbili za rangi moja zilizo nzuri na_ kanzu iliyikuwa na pindo la hariri, alikuwa akitoka miongoni mwa watu wa Banu Sahm, nao walikuwa ni marafiki Wakati wa Ujahilia, akamuuliza \u201cUna nini?\u201d Akamjibu kuwa, Jamaa zako wamedai kuwa wataniua kwa sababu nim\u00e9ingia katika Uislamu. Nae akamwambia, \u2019Basi usihofu, maana sasa hakuna njia ya kukufikia hilo tena baada ya kulisema kwangu&nbsp; umekuwa katika amani.\u2019 Al-\u2018As akatoka na kukutana na watu jangwani, akawauliza; \u201dMmekusudia kwenda wapi?\u201d &#8216;-Nakajibu, \u201dKwa <span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Al-Khattab<\/span> ambaye ametoka katika dini.\u201d <span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Al-\u2018As<\/span> akawaeleza kuwa, \u2019Hakuna njia ya kumuendea kumdhuru&#8217;, hivyo wakamuacha na kutawanyika. (4)<\/p>\n<p class=\"aya_text\" style=\"text-align: left;\">Katika mapokezi ya Ibnu Ishaq anasema: \u201dWallahi,.walikuwa kama watu waliokuwa wamevaa nguo na Wakavuliwa kwa aibu iliyowafika&nbsp; kwa kuadhirika kwao. (5)<\/p>\n<p class=\"aya_text\" style=\"text-align: left;\">Baada ya hapo Mushrikina wa Makka hawakumfanya kitu tena &#8220;Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake). Mujahid amekeoa kutoka kwa Ibn Abbas ya kuwa &#8220;Nilimuliza \u2018Umar bin Al-Khattab, kwa sababu gani ameitwa Al-Faruq?\u201d (yaani mwenye kutenganisha baina ya haki na batili). Nae akamjibu kuwa, Hamza alisilimu kabla yangu kwa siku tatu, kisha akanisimulia kisa cha kusilimul kwake, na mwishoni mwake akasema kuniambia: Wakati niliposilimu nilimwuliza Mtume (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>), \u201cEwe Mtume wa Mwenyezi Mungu (<span style=\"color: #008000;\">\ufdfa<\/span>) hivi sisi si tupo katika njia ya haki tukifa au tukiwa hai?.\u201d Akajibu; bila shaka tupo katika haki<\/p>\n<p>na akaendelea kusema: \u201dNinaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko katika Qudra Yake, kwa hakika nyinyi mko katika haki mkiwa hai\u2018 au mmekufa\u201d Nikauliza, \u201cKwa nini, tunalingania kwa siri?, Ninaapa kwa Yule Ambaye_ Amekutuma na ukweli, kwa hakika lutatoka na kuutangaza Uislamu wetu hadharani.&#8221; Baada ya hapo tukatoka katika safu mbili Hamza akiongoza safu moja na mimi nikiongoza safu ya pili. Tulikwenda mpaka tukaingia msikitini mchana kweupe na mara Mushrikina wa Kikuraishi kutuona sisi (mimi na Hamza) ikawachukiza hali hiyo na kuwapa huzuni ambayo haijawahi kuwapata mfano wake. Siku hiyo ndiyo Mtume wa Mwenyezi Mungu akaniita mimi Al-Faruuq&#8221; <span style=\"color: #ff6600;\">Ibn Masoud<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa akisema: &#8220;&#8216;Hatukuwa tukiweza kusali mbele ya Al-Ka&#8217;aba mpaka \u2018Umar aliposilimu\u201d,(5)<\/p>\n<p>Imepokewa kutoka kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Suhayb bin Sinan Al- Roumy<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) alisema kuwa; \u2019Wakati \u2018Umar aliposilimu ulidhihiri Uislamu na ukawa unalinganiwa bila ya kificho na tukawa&#8217; fukikaa pembezoni mwa Al-Ka\u2019aba tukifanya ibada zetu. Tulilipiza kisasi kwa yule aliyetufanyia uzito na tukamrudishia baadhi ya yale aliyokuwa akitufanyia.\u2019<\/p>\n<p>Imepokewa kutoka kwa <span style=\"color: #ff6600;\">Abdallah bin Masoud<\/span> (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa amesema: (Kutokea siku aliposilimu Umarr tulianza kupata nguvu. (6)<\/p>\n<div>\n<hr>\n<\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>1) Ibid Juzuu 1, Uk 349-350<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>2) Tarikh Umar bin Khattab Uk. 8,<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>3) Ibid Uk 8 Ibn Hashim Juzuu 1, Uk 348-349<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>4) Sahihi Bukhari Juzuu,1 Uk 545<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>5) Ibnu Hisham Juzuu Uk 349<\/em><\/span><\/div>\n<div><span style=\"color: #ff6600;\"><em>6) Sahihi Bukhari Juzuu,1 Uk 349<\/em><\/span><\/div>\n<hr>","protected":false},"excerpt":{"rendered":"<p>AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM &#8216;Umar bin Al-Khattab (Radhi za Allah ziwe juu yake) alikuwa ni mtu mwenye kuhieshimika mno na asiyechezewa, kwa hakika kusiliimu kwake kuliibua vurugu na kuwagonganisha Mushirikina na kuwafanya kuwa ni wanyonge na dhalili. Kukawavika Waislarnu nguvu, utukufu na furaha. Ibn Ishaq amepokea kutoka kwa &#8220;Umar (Radhi za Allah ziwe juu yake) kuwa; \u201dWakati [&hellip;]<\/p>","protected":false},"author":2,"featured_media":15476,"comment_status":"closed","ping_status":"closed","sticky":false,"template":"","format":"standard","meta":{"_acf_changed":false,"give_campaign_id":0,"_bbp_topic_count":0,"_bbp_reply_count":0,"_bbp_total_topic_count":0,"_bbp_total_reply_count":0,"_bbp_voice_count":0,"_bbp_anonymous_reply_count":0,"_bbp_topic_count_hidden":0,"_bbp_reply_count_hidden":0,"_bbp_forum_subforum_count":0,"footnotes":""},"categories":[57],"tags":[],"class_list":["post-16891","post","type-post","status-publish","format-standard","has-post-thumbnail","hentry","category-sera-ya-mtume"],"acf":[],"_links":{"self":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/16891","targetHints":{"allow":["GET"]}}],"collection":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts"}],"about":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/types\/post"}],"author":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/users\/2"}],"replies":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/comments?post=16891"}],"version-history":[{"count":13,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/16891\/revisions"}],"predecessor-version":[{"id":17568,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/posts\/16891\/revisions\/17568"}],"wp:featuredmedia":[{"embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media\/15476"}],"wp:attachment":[{"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/media?parent=16891"}],"wp:term":[{"taxonomy":"category","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/categories?post=16891"},{"taxonomy":"post_tag","embeddable":true,"href":"https:\/\/uongofu.com\/en\/wp-json\/wp\/v2\/tags?post=16891"}],"curies":[{"name":"wp","href":"https:\/\/api.w.org\/{rel}","templated":true}]}}