See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

HUYU NDIYE YATIMA WA KIISLAMU


 ما آثار كفالة اليتيم على المجتمع


Kumuangalia yatima kwa wema ni ishara ya imani , ibashirie kheyri jamii inayojishuhulisha na kutatua matatizo ya mayatima , na kila mwenye kuyafanya haya atakuwa jirani na bwana Mtume Muhammad katika pepo ya ALLAH aliyetukuka kwa mujibu wa hadithi sahihi zilivopokelewa na Imamu Bukhari na Tirmidhiy na Abuu Daud.


قال النبي صلى الله عليه وسلم: "أنا وكافل اليتيم في الجنة هكذا- أي متجاورين- وأشار بأصبعيه السبابة والوسطى" رواه البخاري والترمذي وأبو داود
 

Amesema bwana mtume Muhammad ﷺ: [Mimi na mwenye kumsimamia yatima katika pepo tutakuwa hivi , yani majirani , akaashiria kwa vidole vyake kidole cha shahada na cha kati] [Imepokelewa na Imam Albukhari , Tirmidhy na Abu-Daud.]

Yapendeza kupapasa kichwa cha yatima na kuongea naye kwa upole na huruma ili ahisi kuwa ni mmoja katika jamii yake na kumjali , mambo kama haya ni yenye kupunguza fikra na mawazo kwa yatima na huzalisha furaha baina yake na mwenye kumlea.


وروى الإمام أحمد أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يمسح رأس اليتيم ثلاثاً ويدعو له بالخير والبر

 

Imepokelewa na imam Ahmad kwamba bwana Mtume Muhammad [alikuwa akipangusa kichwa cha yatima mara tatu na akimuombea kheyri na utukufu ].  [Imepokelewa na Imamu Ahmad.]
Uislamu umeweka mikakati ya kidharura ya kuzisimamia mali za mayatima kwa njia ya mirathi au zawadi , mwenye kuzisimamia mali hizi anatakiwa azikuze kwa njia ya kuuza na kununua ili ziongezeke , na isipokuzwa mali hii huenda ikaisha kwa ajili ya kutolewa zaka kila mwaka kabla ya mtoto kubaleghe na kukabidhiwa mali yake .


[قال النبي صلى الله عليه وسلم فيما يرويه الطبراني: [اتجروا في مال اليتيم حتى لا تأكله الصدقة

Amesema bwana Mtume Muhammad  katika hadithi iliyopokelewa na imam Atwabraany , [Fanyeni biashara katika mali ya mayatima ili zisiliwe na sadaka.] 
Yani zisiliwe na zaka ya mwaka baada ya mwaka .
Haifai kwa muislamu yeyote kutumia mali ya mayatima kwa njia ya dhulma na ALLAH aliyetukuka kakemea juu ya hilo na kamuandalia adhabu kali kwa atakayeitumia mali ya mayatima kinyume na utaratibu uliowekwa .

 

قال تعالى : {إن الذين يأكلون أموال اليتامى ظلما إنما يأكلون في بطونهم ناراً وسيصلون سعيراً }     النساء: الآية 9

 

Amesema ALLAH aliyetukuka[hakika wale wanaokula mali ya mayatima kwa njia ya dhulma , bila shaka wanakula moto matumboni mwao , na wataungua katika huo moto wa jahannam uwakao] . [surat annisaa aya ya 9.]

Mwisho

©Abu-Khalfan Assarawi
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. / This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
+255656333678
15/03/17


 

bibaner


Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

5256596
TodayToday3802
Highest 01-09-2020 : 9039
US
Guests 212

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Makkah

title_5e25db1e8aeb114497481131579539230  
title_5e25db1e8af6c15964105021579539230  
title_5e25db1e8b022238601371579539230  

 

 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

title_5e25db1eaf39914456390621579539230
title_5e25db1eaf45d315438291579539230

HUDUMA MPYA

: 3 + 14 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com