See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

SOMO LA FIQHI


 MADINISuali: Madini ni nini? na inamanisha nini ya Hazina iliyozikwa ardhini?

Jawabu: Madini ni chochote kinachotolewa ndani ya ardhi ambacho kwamba sio sampuli ya ardhi kama vile dhahabu, fedha, vyuma, na vijiwe vya tunu kama vile almasi na rubi, na risasi, na vyenginevyo katika vitu asili vinavyotolewa ndani ya Ardhi.

Hazina iliyozikwa ardhini
Ni Mali iliyozikwa ndani ya ardhi kwa kuekwa na mtu, kutokana na dhahabu, na fedha, na mfano wa vitu hivi.

Suala: Ni ipi Hukumu ya zaka ya madini na hazina iliyozikwa ardhini
Jawabu: Hukmu yake ni lazima, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ}   البقرة:267}

 

[Enyi mlioamini! Toeni katika vile vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyokutoleeni katika ardhi] [Al-Baqarah: 267]

Na kauli ya Mtume ﷺ:

 

وفي الركاز الخمس]  رواه البخاري ومسلم]

 

[Na katika hazina iliyozikwa ardhini (toeni) khumusi (1/5))]   [Imepokewa na Bukharin a Muslim.]

Sauli: Ni yapi Masharti ya kutoa zaka ya hazina iliyozikwa ardhini
Jawabu: Hakuna masharti yoyote ya zaka ya hazina iliyozikwa ardhini, basi atakapomiliki mtu hio hazina iliyozikwa ardhini anafaa kutoa zaka yake moja kwa moja.

Kiwango cha kuwajibika mtu kutoa zaka ya madini na hazina iliyozikwa ardhini
Ni wajibu mtu kutoa khumusu (1/5) kwa kichache au kingi atakachopata katika madini na hazina iliyozikwa ardhini, kwa jumla ya kauli ya Mtume ﷺ:

 

وفي الركاز الخمس]  رواه البخاري ومسلم]

 

[Na katika hazina iliyozikwa ardhini (toeni) khumusi]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]


logompya


Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

5969095
TodayToday3557
Highest 04-08-2020 : 8638
US
Guests 168

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Masomo

title_5e9072a2a518c9962037841586524834
title_5e9072a2a52169989890961586524834
title_5e9072a2a529c12137820071586524834
 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

title_5e9072a296f6b14157163831586524834
title_5e9072a297017545280531586524834

HUDUMA MPYA

: 1 + 9 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com