See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

SOMO LA FIQHI


 hikma ya zaka


Suali: Ni ipi hikma ya kuwajibisha kutoa Zaka?

Jawabu: Hekima ya watu kuwajibika kutoa Zaka ni kama zifuatavyo:
1. Ni kuzisafisha nafsi na kuzitakasa kutokana na ubakhili, na madhambi, na makosa, Anasema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

 

خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ}    التوبة:103}

 

[Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo, na uwaombee rehema. Hakika maombi yako ni utulivu kwao]     [suratu At-Tawbah: 103]

2. Kusafisha mali na kuikuza, na kutia baraka ndani yake, kwa kauli ya Mtume ﷺ:

 

ما نقصت صدقة من مال}     رواه مسلم}

 

[Sadaka haipunguzi chochote (inapotolewa) katika mali]     [Imepokewa na Muslim.].

3. Ni mja kupewa mtihani katika kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu, na katika kutanguliza mapenzi yake kwa Mungu zaidi kuliko mapenzi yake ya kupenda mali.

4. Kuwaliwaza mafakiri na kuziba pengo la mahitaji ya wenye haja, jambo ambalo linaongeza mapenzi, na linatimiliza kiwango cha juu sana katika usaidizi wa kijamii baina ya waislamu wa eneo moja.

5. Kujizoezesha katika kutoa kwa njia ya Mwenyezi Mungu.

 

FADHLA YA KUTOA ZAKA

 

Suali: Ni zipi Fadhla ya kutoa zaka?

Jawabu: Fadhlaya kutoa zaka ni kama zi fuatavyo:

1. Ni sababu ya kupata Rehema za Mwenyezi Mungu, Anasema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

 

وَرَحْمَتِي وَسِعَتْ كُلَّ شَيْءٍ ۚ فَسَأَكْتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِنَا يُؤْمِنُونَ}    الأعراف:156}

 

[Na rehema yangu inaweza kukienea kila kitu. Lakini nitawaandikia (kweli kweli kabisa) wale wanaojikinga na yale niliyowakataza, na wanaotoa Zaka na wanaoziamini Aya zetu]       [Al-A’raf: 156]

2. Ni sharti ya kupatikana Nusra ya Mwenyezi Mungu, Anasema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

 

وَلَيَنصُرَنَّ اللَّهُ مَن يَنصُرُهُ ۗ إِنَّ اللَّهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌالَّذِينَ إِن مَّكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنكَرِ ۗ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ

[Na bila shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anayesaidia dini yake.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye kushinda. Wale ambao tukiwamakinisha, (tukiwaweka uzuri) katika ardhi husimamisha Swala na wakatoa Zaka]      [Al-hajj 40-41]

3. Ni sababu ya kufutiwa madhambi, Amesema Mtume ﷺ:

 

وَالصَّدَقَةُ تُطْفِئُ الْخَطِيئَةَ كَمَا يُطْفِئُ الْمَاءُ النَّارَ]    رواه الترمذي]

 

[Na sadaka hufuta madhambi kama vile maji yanavyozima moto]    [Imepokewa na Tirmidhi.].


logompya


Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

5945567
TodayToday5272
Highest 04-03-2020 : 8408
US
Guests 88

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Masomo

title_5e8cce86a590716603220711586286214
title_5e8cce86a599c4217744901586286214
title_5e8cce86a5a295370685001586286214
 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

title_5e8cce86d49aa17086309221586286214
title_5e8cce86d4a767585556061586286214

HUDUMA MPYA

: 9 + 4 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com