See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

SOMO LA FIQHI


HADYU


Maana ya mnyama wa tunu:
Ni wanyama hoa wanaotunukiwa sehemu takatifu kwa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, au ilio wajibishwa kwa sababu ya Tamattu’au Qiraan au kufungizika

Aina ya wanyama wanaotunukiwa

1. Tunuku ya Tamattu na Qiraan
Anayechanganya Hija na Umra kwa njia ya Tamattu au Qiraan itamlazimu achinje Mnyama wa tunuku: naye ni Mbuzi au fungu moja la mafungu saba ya Ngamia au Ngombe. Akikosa mnyama atafunga siku kumi, siku tatu ziwe katika Hija na siku saba ziwe baada ya mwenye kuhiji kurudi kwa watu wake. Hili humlazimu yule ambaye si mkazi wa Makka, iwapo ni miongoni mwa wakazi wa Makka, hatalazimika kuchinja Mnyama wa kutunuku wala kufunga, kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

فَمَن تَمَتَّعَ بِٱلۡعُمۡرَةِ إِلَى ٱلۡحَجِّ فَمَا ٱسۡتَيۡسَرَ مِنَ ٱلۡهَدۡيِۚ فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ ثَلَٰثَةِ أَيَّامٖ فِي ٱلۡحَجِّ وَسَبۡعَةٍ إِذَا رَجَعۡتُمۡۗ تِلۡكَ عَشَرَةٞ كَامِلَةٞۗ ذَٰلِكَ لِمَن لَّمۡ يَكُنۡ  أَهۡلُهُۥ حَاضِرِي ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ     البقرة:196 

 

[Mwenye kujistarehesha kwa Umra mpaka Hija, basi itamlazimu achinje mnyama wa kutunuku aliye sahali kwake, na asipopata atafunga siku tatu katika Hija na saba mtakaporudi. Hizo ni kumi kamili. Hukumu hiyo inamhusu yule ambaye watu wake wa nyumbani si wakazi wa maeneo ya Msikiti wa Haram]    [2: 196].

2. Mnyama wa kutunuku wa kujiotolea
Naye ni mnyama ambaye mwenye kuhiji  au anayefanya Umra Akajitolea kutoa tunuku, mwenye kufanya Hija ya Qiraan au ya Tamattu anamtunuku kwa kutoa zaidi ya wajibu, au ni mnyama ambye hutunukiwa Makka na mtu ambaye hako kwenye ihramu kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

Mnyama anayetunukiwa kwa kujitolea na yule wa Hija ya Tamattu’ au Qiraan, inafaa kwa yule anayemtoa kula kitu katika nyama yake, bali ni sunna kufanya hivyo. Hii ni kuambatana na kitendo cha Mtume  kwa kuwa:

 

أَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ مِنْ كُلِ بَدَنَةٍ بِبَضْعَةٍ فَطُبِخَتْ وَشَرِبَ مِنْ مَرَقِهَا]     رواه الترمذي]

 

 [Aliamrisha Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ katika kila mnyama aliyemtoa kuchinjwa, Basi ikapikwa na akanywa supu yake]    [Imepokewa na Tirmidhi]

3. Kuchinja mnyama wa kutunuku kwa kuzuiliwa kuhiji

Ihswaar: Ni kuzuiliwa kutimiza Hija au Umra au yote mawili. Mwenye kuhirimia Hija au Umra, akazuiliwa na adui kuifikia Alkaaba, au akatukiwa na jambo likamfanya asiweze kufika kwenye Alkaaba, basi atachinja Mnyama mahali alipo, kisha atajitoa kwenye vikwazo vya ihramu, kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

 

فَإِنۡ أُحۡصِرۡتُمۡ فَمَا ٱسۡتَيۡسَرَ مِنَ ٱلۡهَدۡيِۖ }  البقرة: 196}

 

[Basi mkizuilika kuendelea na (ibada ya Hija au Umra,) chinjeni kilichokuwa sahali]  [2: 196].

Na wanyama wa kuchinjwa kwa sababu ya kuzuilika ni Mbuzi/kondoo au fungu moja kati ya mafungu saba ya Ngamia au Ng’ombe.

Mahali pa kuchinja mnyama wa kutunuku
Tunuku ya Hija ya Tamatta’ au Qiraan au ya kujitolea, huchinjwa ndani ya mipaka ya Haram na hugawiwa masikini wake. Iwapo atachinja nje ya mipaka ya Haram haitomtosheleza.

Na mnyama wa tunuku kwa sababu ya kuzuiliwa atamchinja mahali alipozuilika.

Wakati wa kuchinja mnyama wa kutunuku

1. Tunuku ya Hijja ya Tamattu’ Qiraan na ya kujitolea

Wakati wake unaanza baada ya Swala ya Iddi ya siku ya Idd mpaka jua la siku ya mwisho ya siku za Tashriiq kuzama, nayo ni siku ya 13.

2. Tunuku ya kuzuilika

Wakati wake ni pale kizuizi kinapotokea

Miongoni mwa hukumu za Hadyi (Kuchinja mnyma)
Inafaa kwa mwenye kuhiji kumuwakilisha mtu wa kumchinjia ikiwa Hijja yake ni ya Qiraan au Tamattu na akiwa aliyewakilishwa ni mwaminifu. Na lililo bora ni kuwa mwenye kuhiji afanye mwenyewe kwa kuwa Mtume ndivyo alivyofanya.

Fidia haitoshelezi iwe ni badala ya kudhahi, kwa kuwa fidia ni ya kuchanganya Hija na Umra, ama kudhahi ni sunna ya anayehiji na asiyehiji.


logompya


Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6859950
TodayToday2919
Highest 06-25-2020 : 11527
US
Guests 255

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Masomo

title_5f004dda8f67515618277651593855450
title_5f004dda8f71117946406091593855450
title_5f004dda8f7a918821247341593855450
 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

title_5f004ddae0bf710737381681593855450
title_5f004ddae0c8d4695529741593855450

HUDUMA MPYA

: 7 + 6 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com