See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


637


Ibni Hajar anasema: 'Kukatika kwa Wahyi kulikuwa kumekusudiwa kumuandaa Mtume na kumuondoa khofu aliyokuwa nayo, na ili ipatikane shauku ya kurejea huo wahyi.(1)

Baada ya kuondoka kwa vivuli vya kuoteshwa na zikathibiti alama za uhakika na Mtume akajua kwa yakini kuwa amekuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu Aliye Mkuu na Mtukufu, na kuwa aliyemjia ni Mjumbe wa mbinguni aliyetumwa kumletea khabari kutoka kwa Mwenyezi Mungu . Ikawa kutazamia kwake kuja kwa Wahyi ni sababu ya kuongezeka yakini; na uvumilivu wake ni maandalizi ya Wahyi kurejea. Jibril alimjia kwa mara ya pili. Bukhari amepokea kutoka kwa Jabir bin Abdillahi, kuwa yeye alimsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akizungurnzia kukatika kwa wahyi: "Wakati ninakuienda, ghafla nilisikia sa uti kutoka mbinguni nikanyanyua macho yangu na kutazama mbinguni, nikamwona Malaika ambaye alinijia kaiika pango la Hiraa amekaa juu ya kiti, katikati ya mbingu na ardhi, nikapiga magoti na kuporomoka mpaka kwenye ardhi, niliposimama nikarudi nyumbani ninatetemeka. Nikisema, 'Nifunikeni, Nifunikeni, wakanifunika, na hapo Mwenyezi Mungu ﷺ Akateremsha Sura:

 

{يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ  قُمْ فَأَنذِرْ  وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ  وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ  وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ}

 

[Ewe Uliyejifunika maguo. Simama uonye (viumbe). Na Mola wako umtukuze. Na nguo zako uzisafishe. Na mabaya yapuuze.]      [Al-Muddaththir:1-5]

kisha Wahyi ukawa unakuja kwa nguvu,' mfululizo na 
kufuatana.(2) *


1) Fathul Bari, Juzuu 1, Uk. 27.
2) Sahihil Bukhari, Kitab Ttafsir, Babu Rrijz Fahjur, [uzuu 2, Uk. 733.]

*Arraheeq Al Makhtum 108


bibaner


Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

4953708
TodayToday10240
Highest 12-05-2019 : 10918
US
Guests 93

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Makkah

title_5df1b78406b6f3713342681576122244  
title_5df1b78406be412506486921576122244  
title_5df1b78406c6c9728211681576122244  

 

 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

title_5df1b7843da5c5860478231576122244
title_5df1b7843dacc17865064061576122244

HUDUMA MPYA

: 2 + 2 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com