See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

KITAAB AT-TAWHIID


kitabu tawhid


{باب 17 قول الله تعالى : {إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ

:قَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى

{إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ }

وَفِي اَلصَّحِيحِ، عَنْ اِبْنِ الْمُسَيَّبِ، عَنْ أَبِيهِ، قَالَ: لَمَّا حَضَرَتْ أَبَا طَالِبٍ الْوَفَاةُ; جَاءَهُ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) وَعِنْدَهُ عَبْدُ اَللَّهِ بْنُ أَبِي أُمِّيَّةَ وَأَبُو جَهْلٍ فَقَالَ لَهُ: [يَا عَمِّ قُلْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ كَلِمَةً أُحَاجُّ لَكَ بِهَا عِنْدَ اَللَّهِ] فَقَالاَ لَهُ: أَتَرْغَبُ عَنْ مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ؟ فَأَعَادَ عَلَيْهِ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَأَعَادَا، فَكَانَ آخَرَ مَا قَالَ: هُوَ عَلَى مِلَّةِ عَبْدِ الْمُطَّلِبِ، وَأَبَى أَنْ يَقُولَ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اَللَّهُ فَقَالَ اَلنَّبِيُّ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ مَا لَمْ أُنْهَ عَنْكَ)). فَأَنْزَلَ اَللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: {مَا كَانَ لِلنَّبِيِّ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَن يَسْتَغْفِرُوا لِلْمُشْرِكِينَ وَلَوْ كَانُوا أُولِي قُرْبَىٰ} وَأَنْزَلَ اَللَّهُ فِي أَبِي طَالِبٍ: {إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ

إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ


MLANGO WA 17 NENO LAKE MWENYEZI MUNGU [KWA HAKIKA WEWE HUMWONGOI UMPENDAE]


Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao]  [Al-Qasas: 56]

Katika Sahihi (Al Bukhari), kutoka kwa Ibn Musayyib amehadithia kutoka kwa baba yake: Mauti yalipomkaribia Abuu Twaalib, Mtume  wa Mwenyezi Mungu alimwendea akamkuta ‘Abdullaah bin Abiy Umayyah na Abuu Jahl wakiwa pamoja naye. Mungu  akamwambia: [Ewe ‘ammi yangu! Sema laa ilaaha illa-Allaah, hivyo utaniwezesha kukuombea shafaa (uombezi) mbele ya Mwenyezi Mungu] Wawili hao wakamwambia: Utaacha dini ya [baba yako] ‘Abdul-Muttwalib?  Mtume wa Mungu ﷺ akakariri na wawili hao wakakariri nao vile vile. Ikawa neno la mwisho alosema ni kubakika katika dini ya ‘Abdul-Muttwalib. Akafariki akiwa amekataa kusema ‘Laa ilaaha illa-Allaah’. Mtume  akasema: [Nitaendelea kukuombea maghfirah madamu sijakatazwa kufanya hivyo]. Hapo Mwenyezi Mungu Akateremsha Aya hii: [Haimpasii Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni.] [At-Tawba: 113] Kisha Akateremsha kuhusu Abuu Twaalib: [Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao]  [Al-Qaswas: 56]

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1.Tafsiri ya Ayahkatika Suwrah Al-Qaswas: 56

[Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye. Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao]

2. Tafsiri ya Aya:

[Haimpasii Nabii na wale walio amini kuwatakia msamaha washirikina, ijapo kuwa ni jamaa zao, baada ya kwisha bainika kuwa hao ni watu wa Motoni.]  [At-Tawbah113].

3. Suala kubwa la tafsiri ya kauli yake Mtume : [Sema, Laa ilaaha illaa Allaah] Inakinzana na madai ya wanodai kuwa wana ujuzi wa elimu ya Dini (kudai kwao kwamba kuitamka kwake inatosheleza kusamehewa juu ya kwamba wanawaomba na kuwaabudu mawalii wao).

4. Abuu Jahl na wenzake walijua kusudio la Mtume alipomwambia Abuu Twaalib: [Sema ‘Laa ilaaha illaa Allaah)), Basi Mwenyezi Mungu  Amdhalilishe yeyote ambaye elimu yake juu ya asili ya Uislamu ni ndogo kuliko ile ya Abuu Jahl.

5. Hima ya Mtume kutaka kumsilimisha ‘ammi yake.

6. Kukanushwa yeyote anayedai kuwa ‘Abdul-Muttwalib na baba zake walikuwa Waislamu.

7. Mtume  alimwombea ‘Ammi yake msamaha lakini hakusamehewa, na kuwa hilo limekatazwa.

8. Madhara ya kuandamana na waovu.

9. Madhara ya kuwatukuza kibubusa viongozi na wahenga (na hali ni washirikina).

10. Shubuha za wapotofu katika hilo ni hoja za ujaahiliyyah (kama Abuu Jahl alivyojitokeza).

11. Dalili kwamba ‘amali za mmja zinategemea mwisho wake, kwa sababu kama angeitamka laa ilaaha illa-Allaah, angeliokoka.

12. Zingatio la hoja hii ya mwisho katika nyoyo za wapotofu kujivunia dini na mila za mababu, kwa sababu kisa kinathibitisha kwamba hawakujadiliana naye isipokuwa kuhusu kuing’ang’ania dini au mila zao, japokuwa Mtume aliendelea kumbembeleza Abuu Twaalib atamke shahaada, kwani angelishuhudia angeliokoka, lakini wao wakashikilia tu umuhimu wa kufuata dini ya wazazi wao.


bibaner


Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

4560554
TodayToday8274
Highest 10-22-2019 : 10683
US
Guests 164

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Makkah

title_5db10bbc3d6842932121041571883964  
title_5db10bbc3d71a678317441571883964  
title_5db10bbc3d7a69589590781571883964  

 

 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

 
title_5db10bbc60c553698335701571883964

HUDUMA MPYA

: 13 + 2 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com