See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

KITAAB AT-TAWHIID


kitabu tawhid


باب ما جاء في الرقى والتمائم

في الصحيح عن أبي بشير الأنصاري رضي الله عنه [ أنه كان مع رسول الله صلى الله عليه وسلم في بعض أسفاره ; فأرسل رسولا أن لا يبقين في رقبة بعير قلادة من وتر، أو قلادة إلا قطعت
وعن ابن مسعود رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: [ إن الرقى والتمائم والتولة شرك ]  رواه أحمد وأبو داود
" التمائم ": شيء يعلق على الأولاد من العين ؛ لكن إذا كان المعلَّق من القرآن فرخص فيه بعض السلف، وبعضهم لم يرخص فيه، ويجعله من المنهي عنه، منهم ابن مسعود رضي الله عنه
و" الرقى ": هي التي تسمى العزائم، وخص منها الدليل ما خلا من الشرك رخص فيه رسول الله صلى الله عليه وسلم من العين والحمة.و " التولة ": شيء يصنعونه يزعمون أنه يحبب المرأة إلى زوجها، والرجل إلى امرأته
وعن عبد الله بن عكيم مرفوعا: "من تعلق شيئا وُكل إليه"   رواه أحمد والترمذي
وروى أحمد عن رويفع قال: قال لي رسول الله صلى الله عليه وسلم: [يا رويفع، لعل الحياة ستطول، بك فأخبر الناس أن من عقد لحيته، أو تقلد وترا، أو استنجى برجيع دابة أو عظم، فإن محمدا بريء منه
وعن سعيد بن جبير قال: "من قطع تميمة من إنسان كان كعدل رقبة". رواه وكيع. وله عن إبراهيم 3 قال: [ كانوا يكرهون التمائم كلها، من القرآن وغير القرآن
فيه مسائل
الأولي: تفسير الرقى والتمائم
الثانية: تفسير التولة
الثالثة: أن هذه الثلاث كلها من الشرك من غير استثناء
الرابعة: أن الرقية بالكلام الحق من العين والحمة ليس من ذلك.الخامسة: أن التميمة إذا كانت من القرآن فقد اختلف العلماء: هل هي من ذلك أوْ لا؟
السادسة: أن تعليق الأوتار على الدواب عن العين من ذلك
السابعة: الوعيد الشديد على من تعلق وترا
الثامنة: فضل ثواب من قطع تميمة من إنسان
التاسعة: أن كلام إبراهيم لا يخالف ما تقدم من الاختلاف، لأن مراده أصحاب عبد الله بن مسعود


MLANGO WA 07 YALIKUJA KUHUSU ZUNGUO NA HIRIZI


Katika Sahih, (ya Bukhari) Imepokelewa jutoka kwa Abuu Bashiyr Al-Answaariyy (Radhi za Alla ziwe juu yake) kwamba alikuwa pamoja na Mtume ﷺ katika safari mojawapo. Akamtuma mjumbe kuamrisha kwamba: [Kusiachwe kidani cha uzi au kidani chochote katika shingo za ngamia isipokuwa kikatwe]     [Imepokewa na Bukhaariy na Muslim]

Na Imepokelewa kutoka kwa Ibn Mas’uwd (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba Nimemsikia Mtume  wa Mwenyezi Mungu  akisema: [Hakika Ar-Ruqaa, At-Tamaaim na At-Tiwalah zote ni shirki]    [Imepokewa na Ahmad, Abuu Daawuwd]

At-Tamaaim: Hirizi Wanachofungwa watoto shingoni (au mkononi) kukinga jicho baya.  Lakini ikiwa kinachofungwa ni kutokana na Qur'ani Baadhi ya Salaf Swaalih (Wema waliotutnagulia) wameruhu, na wengine wamekataza. Na Ibn Mas’uwd ni miongoni mwa waliokataza.

Ar-Ruqaa : Na ndio inayoitwa Al-‘Azaaim: Zunguo. Dalili imehusisha ile isiokuwa na Ushirikina. Mtume  wa Mwenyezi Mungu  ameiruhusu (zunguo) mtu anapopatwa na jicho baya (au hasad) au homa.

At-Tiwalah: Kinachodaiwa kuwa kinasababisha mwanamke apendwe zaidi na mumeme au mume apendwe zaidi na mkewe.

Na Hadith  Marfuw’  kutoka kwa Mtume  Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Hukaym: [Atakayetundika kitu basi amejiweka katika ulinzi wa hicho kitu alichokivaa] [Imepokewa na Ahmad na At-Tirmidhiy]

Na amepokea Ahmad kutoka kwa Ruwayfi’  ambaye amesema: Ameniambia mimi  Mtume : [Ewe Ruwayfi’! Huenda ukaishi zaidi baada yangu. Kwa hiyo wajulishe watu kwamba: Yeyote atakayefunga fundo ndevu zake, au akaweka nyuzi au mshipi shingoni mwake [kuwa ni talasimu] au akastanji kwa choo cha mnyama au mfupa, basi Muhammad yuko mbali na yeye ]    [Imepokewa na Ahmad, Abuu Dawud]

Kutoka kwa Sa’iyd bin Jubayr amesema: [Atakayekata hirizi iliyovaliwa na mtu, ni kama Alieacha Mtumwa Huru .]  Amepokewa na Wakiy’  na pia amepokea toka kwa Ibrahim ambaye amesema: “Walikuwa (salaf) wakichukia Hirizi zote ziwe (zimeandikwa kwa) Qur'ani na zisizokuwa za Qur'ani ”  walikuwa hao ni sahibu wa Ibn Mas’uwd (Radhi za Allah ziwe juu yake.

Masuala Muhimu Yaliyomo:

1- Tafsiri kuhusu Zunguo na Hirizi.

2- Tafisiri kuhusu At-Tiwalah.

3- Kwamba Vitu vitatu vyote hivyo ni shirki na hakuna kilicho vuliwa.

4-  Kwamba Ruqyah kwa maneno ya haki (Qur'ani) kwa ajili ya kukinga au kuondosha jicho si shirki.

5- Kwamba Hirizi ikiwa ni kwa Qur'ani, Wanachuoni wametofautiana (kuhusu kutumia hirizi) je ni katika Shirk au la.

6- Kuwavalisha mshipi (wa aina yoyote) wanyama kwa ajili ya kukinga jicho ni katika shirki.

7- Onyo la adhabu kali kwa anayevaa vitu kama hvyo (au kufunga fundo au mshipi wa aina yoyote kwa itikadi kuwa ni kinga au kuondosha madhara.)

8- Fadhila za Thawabu za mtu anayemkata mtu Hirizi.

9- Kauli ya Ibrahim An-Nakha’iyy (kuwa As-Salaf walikuwa wakijiepusha na talasimu hata ikiwa Aya za Qur'ani au chochote,) haipingani na tofauti za rai zilotajwa, kwani maneno hayo yanaashiria msimamo wa wafuasi wa ‘Abdullaah bin Mas’uwd.


logompya


Search Videos

RSS Content

<

 

 

Visitors Counter

6956226
TodayToday9853
Highest 07-11-2020 : 11735
US
Guests 179

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Masomo

title_5f0bbc531d44b16408737831594604627
title_5f0bbc531d51912701209121594604627
title_5f0bbc531d5dc16804258121594604627
 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

title_5f0bbc5384c926971955741594604627
title_5f0bbc5384d2410735284151594604627

HUDUMA MPYA

: 8 + 7 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com