See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

TAWHIYD-UL-ULUUHIYYAH


أهمية توحيد الألوهية


Nayo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika aina zote za ibada sawa za dhahiri au za ndani sawa iwe kauli au kitendo pamoja na kukanusha kufanyiwa ibada chochote kisichokuwa Mwenyezi Mungu.

Na hii aina ya tauhidi ndiyo mitume walitumwa kufikisha na wakawa wanaanza kuwafundisha watu wao hii aina ya tauhidi kwanza. Na Mwenyezi Mungu akateremsha vitabu kwa ajili yake. Na mvutano na mabishano makubwa yakazuka baina ya mitume hawa na umma wao kwa ajili ya hii tauhidi. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ :

 

[ وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ}   [النحل: من الآية 36}

 

[Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani.]   [Annahl aya 36]

Na akasema Mwenyezi Mungu:

 

[ وَمَا أَرْسَلْنَا مِنْ قَبْلِكَ مِنْ رَسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لا إِلَهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ}    [الأنبياء: 25}

 

[Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi.Basi niabuduni Mimi tu.]     [Al-anbiyaa aya 25]


Dalili ya aina hii ya tauhidi ni:


1. Kauli yake Allah :

 

[ إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ}  [الفاتحة:5}

 

[Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada.]     [ Al-fatiha aya 5]

2. Na kauli yake:


[ وَاعْبُدُوا اللَّهَ وَلا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ]    [النساء: من الأية 36]

[Na Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote.]   [Suratun-nisaa aya 36]

3. Na kauli yake Allah:

 

وَلِلَّهِ غَيْبُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَإِلَيْهِ يُرْجَعُ الْأَمْرُ كُلُّهُ فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ ۚ وَمَا رَبُّكَ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ}    هود:123}

 

[Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyo fichikana katika ardhi na mbingu,na mambo yote yatarejezwa kwake. Basi muabudu Yeye na umtegemee Yeye. Na Molawako Mlezi haghafiliki na yale mnayo yatenda.]   [Huud aya 123].

4. Na kauli yake :

قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ  لَا شَرِيكَ لَهُ ۖ وَبِذَٰلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَا أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ}    الأنعام:162-163}

 

[Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, nikwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.163. Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyo amrishwa, na mimi ni wa kwanza wa waislamu.]    [ Anaam 162-163]

5. Kauli yake mtume :

 

قوله صلى الله عليه وسلم لمعاذ بن جبل رضي الله عنه:  يا معاذ، أتدري ما حق الله على العباد؟ وما حق العباد على الله؟ " قال معاذ: الله ورسوله أعلم. قال: "حق الله على العباد: أن يعبدوه ولا يشركوا به شيئا، وحق العباد على الله: أن لا يعذب من لا يشرك به شيئا     رواه البخاري ومسلم

 

[Ewe Muadh, wajua nini haki yake Mwenyezi Mungu juu ya waja(wake)na nini haki ya waja juu ya Mwenyezi Mungu? Akasema(Muadh),Mwenyezi Mungu ndie ajuae na Mtume wake. Akasema :Haki yake Mwenyezi Mungu juu ya waja ni kwamba wamuabudu wala wasimshirikishe Naye chochote, na haki ya waja juu ya Mwenyezi Mungu ni kwamba asimwadhibu (Mwenyezi Mungu)asiyemshirikisha Naye chochote ]    [Imepokewa na Imam Bukhari na Muslim] 


SIKILIZA SHEREHE YA MADA HII NA SHEIKH SALIM KHATIB (1) Chanzo: Tauhidi. Daktari Hajj Makokha Maulid

bibaner


Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

4251518
TodayToday4579
Highest 09-12-2019 : 5912
US
Guests 67

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Makkah

title_5d7ebe839a64914847554411568587395  
title_5d7ebe839a703567457361568587395  
title_5d7ebe839a7bf18484638811568587395  

 

 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

 
title_5d7ebe83b8b9c3688963961568587395

HUDUMA MPYA

: 8 + 2 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com