See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

VIGAWANYO VYA MAJI

SWALI: Maji yanagwanyika sehemu ngapi kama walivyo elezea wanachuoni wa fiqhih?

JAWABU: Maji yanagawanyika Viganyo vitatu kwa ujumla kama walivyo elezea wanachuoni wa fiqih kwa itifaki ya madhehebu manne.
Kigawanyo cha kwanza:Ni maji ya kawaida,nao ni maji yaliobaki katika umbile lake,bila ya kubadilika rangi yake, au harufu yake, au tamu yake,kwa kitu ambacho ni vigumu kuepUkana nacho.
Dalili kutoa kwenye Qur'ani: 

وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً طَهُورًا}     الفرقان:48}

Mwenyezi Mungu asema:

"Na tumeteremsha kutoka Mbinguni maji Twahara"     [Alfuqaan: 48]

Na amesema tena :

 

وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُم مِّنَ السَّمَاءِ مَاءً لِّيُطَهِّرَكُم بِهِ وَيُذْهِبَ عَنكُمْ رِجْزَ الشَّيْطَانِ}    الأنفال:11}

 

[Na akakuteremshieni maji kutoka mbinguni ili kukusafisheni kwayo na kukuondoleeni uchafu wa Shet'ani,"   [Al-Anfaal:11]

Na katika hadithi 


عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه , عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: [ إن الماء طهور لا ينجسه شيئ] رواه أبوداود والترمذي والنسائي وأحمد 

Amepokea Abuu said Al'khudriy Radhi za mwenyezi mungu ziwe juu yake,kutoka kwa Mtume Rehema na amani zimfikie yeye amesema [hakika maji ni twahara na hayanajisiki kwa kitu chochote]  [Imepokewa na Abuu Daud na Attirmidhiy,na Annasai,na Ahmad ]
Na hukumu ya maji haya ni twahara yenyewe na waweza kutwahirishia vitu vingine, nao ni kama maji ya mvua, maji ya kisima, maji ya bahari, maji ya barafu, maji chemchem ya ardhi, maji ya zam zam, na maji yalio badilika kwa kitu kilicho zalikana nao.


Kigawanyo cha pili: Ni maji yalio badilika kwa kuingia kitu twahara na kubadilisha rangi yake, au harufu yake, au tamu yake kama vile maji ya waridi,juice, chai, na kadhalika.
Na hukmu ya maji haya huwa ni twahara yenyewe waweza kutumia katika kunywa na kupikia lakini huwezi kutumia katika kujitwahirisha kama vile kutawadha au kuogea.

Kigawanyo cha tatu: Ni maji yalio najisika ,nao ni maji yalio ingia najisi na kubadilisha moja katika sifa zake kama vile tamu yake au rangi yake au harufu yake.
Na hukumu ya maji haya ni haramu kuyatumia kama kunywa, au kupikia na vile vile ni haramu katumia katika mambo ya ibada kama vile kutawadhia, kuogea na kuoshea.
Na baadhi ya wanachuoni wamegawanya maji Vigawanyo viwili tu.
A) Maji twahara: nao ni maji ya kwaida yalio baki katika umbile lake,
B) Maji ya najisi: Nao ni maji yalio ingia najisi na kubadilisha moja katika sifa zake, kama tamu yake, rangi yake, na harufu yake.

Na Allah ndie Mjuzi zaidi


 

bibaner


Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

4940794
TodayToday6277
Highest 12-05-2019 : 10918
US
Guests 1064

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Makkah

title_5df00d4dca6474140417201576013133  
title_5df00d4dca6e018643992071576013133  
title_5df00d4dca7732852110081576013133  

 

 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

 
title_5df00d4ded35d5682878721576013133

HUDUMA MPYA

: 13 + 10 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com