See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

 

RUHUSA YA KUKUSANYA SWALA KWA MGONJWA

 

Suala; Je mgonjwa alie lala kitandani anaruhusiwa kukusanya Swala na kupunguza?
Jawabu: Mtu akishikwa na ugonjwa na akawa hawezi kusimama kuswali, basi Sheria imemruhusu kuswali kwa kukaa, na ikiwa hawezi kukaa basi aswali kwa ubavu na akishindwa kuswali kwa ubavu basi anaswali kwa kuashiria rukuu na kusujudu na hii ni kwa hadithi ya Imraan bin Huswein asema nilikuwa na bawasili, nikamuliza Mtume ﷺ Kuhusu Swala akasema:

صل قائماً، فإن لم تستطع فقاعداً، فإن لم ‏تستطع فعلى جنب]   رواه الجماعة إلا مسلما] 

[Swali kwa kusimama ikiwa hutoweza basi swali kwa kukaa na ikiwa hutoweza swali kwa ubavu]   [Imepokewa na Jamaa ila Muslim]
Na amejuzisha Imam Ahmad kukusanya swala, sawa kwa kutanguliza au kuakhirisha kwa udhuru wa ugonjwa, kwa sababu ugonjwa uko na shida zaidi kuliko shida ya Mvua.
Na Amesema Imam Annawawiy "ni Huja ya nguvu," yaani Hoja ya Imamu Ahmad
Na imekuja katika kitabu cha Al-Mughniy cha Ibnu Qudaama "Na ugonjwa unao ruhusiwa kukusanya ni ule unao mpatia mtu shida na udhaifu ikwa ataswali kila swala kwa wakati wake"
Na kauli hii ndio inayo kwenda sambamba na sheria yetu kwa sababu shida huleta wepesi.
Ama kupunguza swala kwa kuswali adhuhuri na alasiri na Ishaa rakaa mbili hili halifai kwa sababu lingekuwa lafaa mtume angemruhusu huyu Swahaba Imraan Bin Huswein alipo muuliza pamoja na kuwa Mtume alimruhusu kuacha baadhi ya nguzo kama kusimama kwa ajili ya kumsahilishia na hili lakupunguza kama lafaa basi Mtume  ange mruhusu.


Na Allah ndie Mjuzi zaidi.


bibaner


Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

4122703
TodayToday5935
Highest 08-02-2019 : 7186
US
Guests 158

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Makkah

title_5d58a7cdbc63515231448271566091213  
title_5d58a7cdbc73615841093601566091213  
title_5d58a7cdbc82d7805569281566091213  

 

 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

 
title_5d58a7cddf7259989264201566091213

HUDUMA MPYA

: 4 + 5 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com