See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

 

HUKMU YA MWENYE KUSWALI NA NAJISI KWA KUSAHAU

 

Suali: Ni ipi hukmu ya mwneye kuswali na najisi kwa kusahau ?

Jawabu: Bila shaka mtu kuwa twahara ni katika masharti ya kusihi Swala ya mtu, utwahara wa nguo, na mwili, na sehemu ya kufanya ibada. Kwa hivyo Mwenye kuswali naye ana najisi bila ya kuijua au akaisahau, basi Swala yake ni sahihi. Kwa kuwa ilithubutu kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu aliswali akavua viatu vyake, na watu wakavua viatu vyao. Alipoondoka alisema ﷺ: [kwa nini mlivua viatu vyenu?] Wakasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tulikuona ukivua viatu vyako na sisi tukavua”. Mtume akasema: [Jibrili alinijia akanipasha habari kwamba viatu vina uchafu. Basi anapokuja mmoja wenu msikitini, avigeuze viatu vyake avitazame. Akiona kuwa vina uchafu, basi na avisugue chini kisha aswali navyo.]

[Imepokewa na Abu Daud.]

Na yoyote atakayejua kuwa ana najisi akiwa katikati ya Swala, itamlazimu kuiondoa, kisha aendelee na Swala yake na ajengee juu ya kile alichokiswali.

Na kama mtu ameswali na najisi kisha akakumbuka baada ya kumalizwa swala je ataswali tena ama hatoswali? katika Suala hili wanchuoni wamekhtalifiana juu ya kauli tatu:

kauli ya kwanza: Swala yake ni sahihi wala hatolazimika kuswali tena.

kauli ya pili: Nilazima aswali tena,kwa sababu ameswali akiwa na najisi.

kauli ya tatu: Ataswali ikiwa bado wakati wa Swala haujatoka.

Lakini katika kauli zote hizi tatu, kauli ya sawa, ni kuwa hatowajibika kuswali tena, kwa kutegemea hadithi iliyotangulia kuwa Mtume  aliswali na viatu vikiwa na najisi, na alipo juzwa na Jibriil alayhi salaam alivua viatu na kuendelea na Swala hali yakuwa hakuziregelea rakaa alizo swali na najisi,na hii ni dalili ya kuonyesha ikiwa mtu hajui kama uko na najisi akaswali basi halazimiki kuiregelea Swala yake, na huu ndio msimamo wa Sheikhul-Islamu Ibnu taymiyah na wengineo.

Na allah ndie mjuzi zaidi.

bibaner


Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

5256058
TodayToday3264
Highest 01-09-2020 : 9039
US
Guests 214

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Makkah

title_5e25c9838428515406651961579534723  
title_5e25c9838432313364343071579534723  
title_5e25c983843b414384625221579534723  

 

 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

title_5e25c983a8c5911400462651579534723
title_5e25c983a8d183925674001579534723

HUDUMA MPYA

: 10 + 4 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com