See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

NI MASHATRI GANI YA MTU KULAZIMIKA KUFUNGA?


Suali: Ni yapi Mashrti ya mtu kuwajibika Kufunga Mwezi wa Ramadhani ?

Jawabu: Masharti ya mtu kuwajibika Kufunga ni kama ifuatavyo:
1. Uislamu: Haimlazimu kafiri kufunga,na hata kama atafunga saumu yako haikubaliwi,na vile ile aliye ritadi amali zake hazukubaliwi,kwa neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

 

لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِين}    الزمر:65}

 

"Bila ya shaka ukimshirikisha Mwenyezi Mungu a'mali zako zitaanguka, na lazima utakuwa miongoni mwa wenye kukhasiri."      [Al-Zzumar:65]

kwa sababu Uislamu ni Shari ya kukubaliwa amali ya Mwanadamu.

2. Kubaleghe: Sio lazima kwa mtoto mdogo kufunga, lakini huamrishwa kufunga akiwa anaweza ili kumpa mazoezi ya saumu naye azoee.Kwa neno lake Mtume :

 

رفع القلم عن ثلاثة: الصبي حتى يحتلم والنائم حتى يستيقظ والمجنون حتى يفيق.]     أخرجه أحمد وأبو داود]

 

[Kalamu imeinuliwa juu ya watu watatu,Mtoto mpaka abaleghe,na alielala mpaka aamke,na Mwenda wazimu mpaka apoe]    [Imepokelewa na Ahmad na Abuu Daud]

3. Kuwa na akili: Sio wajibu kwa mwendawazimu kufunga.Kwa hadithi iliyo tangulia

4. Uwezo wa kufunga: Sio wajibu kufunga kwa mtu ambaye hawezi kufunga (labda amekuwa mzee sana ama afya yake haimruhusu kuhimili saumu).Kwa neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

 

وَعَلَى الَّذِينَ يُطِيقُونَهُ فِدْيَةٌ طَعَامُ مِسْكِينٍ}      البقرة:184}

 

"Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini."      [Al-Baqara:184]

5. Kwa Mwanamke asiwe kuwa kwenye ada yake ya Mwezi, au damu yanifasi.ama akiwa katika ada yake ya mwezi au akiwa katika nifasi ni haramu kufunga na watalizimika kula na kulipa wakati mwengine kwa neno lake Bibi Aisha radhi za Allah ziwe juu yake asema:

 

كنا نحيض على عهد رسول الله صلى الله عليه وسلم فنؤمر بقضاء الصيام ولا نؤمر بقضاء الصلاة]   رواه أبوداود]

 

[Tulikuwa tukiingia kwenye hedhi zama za Mtume  tukiamrishwa kulipa Saumu wala hatuamrishwi kulipa Swala]    [Imepokewa na Abuu Daud]


logompya


Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

7238593
TodayToday3668
Highest 07-30-2020 : 13247
US
Guests 304

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Masomo

title_5f2bdcaf5a0678871328041596710063
title_5f2bdcaf5a0d718019111501596710063
title_5f2bdcaf5a16a11324946831596710063
 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

title_5f2bdcaf84b9c1788574281596710063
title_5f2bdcaf84c5a20314812591596710063

HUDUMA MPYA

: 5 + 11 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com