See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

JE ALIEFUNGUA BAADHI YA MASIKU KWA DHARURA ATAPATA FADHLA KAMA ZA YULE ALIFUNGA RAMADHANI KAMILI?


Suali : 

Imekuja katika sahihi mbili katika Hadithi ya Abu hureira Radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume MUHAMMAD ﷺ amesema : [Atakaefunga Ramadhan hali yakua ana imani na anatarajia malipo basi atasamehewa madhambi yake yaliyopita.] jee yule aliyefungua baadhi ya masiku katika ramadhan kwa sababu ya udhuru jee fadhla hii ataipata ? Au fadhla hii ni kwa yule aliefunga ramadhani kamili.

Jawabu :
Ama baada ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na kumswalia Mtume Muhammad ﷺ.
Udhahiri wa Hadithi hii na ALLAH ni mjuzi zaidi ni kwamba fadhla hii inaenea hata kwa yule ambae hakufunga Ramadhani kamili .imekuja katika kitabu cha (Faidhul Qadiir) alipozungumzia hadithi hii ya :

 

مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ]    رواه البخاري ومسلم]

 

[Atakaefunga Ramadhan hali yakua ana imani na anatarajia malipo basi atasamehewa madhambi yake yaliyopita] Anasema Karmaany "Na lau atawacha kufunga katika Ramadhani na nia yake ni kwamba lau sio udhuru uliompata angelifunga basi ataingia katika hukmu hii kama vile akiswali hali yakua amekaa kwa udhuru basi atapata thawabu ya mwenye kusimama". mwisho
Na ALLAH ni mjuzi zaidi.


*Chanzo: Fatawa za Sheikh Al Munajid

Imefasiriwa na Mahamd Fadhil El Shiraziy


bibaner


Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

5275125
TodayToday6352
Highest 01-16-2020 : 8736
US
Guests 237

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Makkah

title_5e28f7695d0cb6675833551579743081  
title_5e28f7695d15c7394078871579743081  
title_5e28f7695d1ec14587537551579743081  

 

 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

title_5e28f7695eb2210856184521579743081
title_5e28f7695ebb710840372951579743081

HUDUMA MPYA

: 15 + 9 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com