See other templatesSee other Balagh Websites

Menu

Dkt. Gary Miller


 garry miller 5


Huyu ni mwanahisabati na mwanatheolojia wa kutokea Canada. Alikuwa akijitolea kufanya kazi za kimishenari za Kikristo katika maisha yake lakini akaja kugundua mambo mengi yenye mashaka katika Biblia. Mwaka 1978 alianza kuisoma Qur’an akitaraji atakutana na mchanganyiko wa ukweli na uongo pia. Aligundua kwa mshangao kuwa ujumbe uliobebwa katika kitabu hiki cha Qur’an unaendana vilivyo na ule ujumbe uliopatikana katika Biblia baada ya kuchujwa. Akawa Muislamu na tangia hapo amekuwa ni mwenye kufanya mihadhara mbali mbali ya umma kuhusu Uislamu akitokea katika redio na televisheni pia. Vile vile ni mtunzi na wa makala nyingi za kiislamu. Akiwa na mtaalamu wa hisabati katika Chuo Kikuu cha Toronto, aghalabu amekuwa ni mwenye kuchambua jambo kwa utaalamu wa hali ya juu. Na hivyo, Gary Miller akafanya uchanganuzi wake kwa aya za Qur’an na matokeo yakawa ni kujisalimisha kwa mtunzi wake. Hii ni moja ya aya za kitabu hiko:

[Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi]   [Q 4:82]

Akiongelea aya hii, Dkt. Miller anasema: “Moja ya kanuni kubwa ya kisayansi ni ile kanuni ya kutafuta makosa, au kuangalia dosari katika nadharia mbalimbali mpaka itapowekwa sawa (Falsification Test). Cha kushangaza kitabu hiki cha Qur’an tukufu kinawauliza Waislamu na wasio Waislamu wajaribu kutafuta makosa ndani yake na kuwahahkikishia kuwa hawatapata hitilafu hata kidogo…Hakuna mwandishi yeyote hapa duniani mwenye ujasiri wa kuandika kitabu na kusema hakina makosa, lakini Qur’an imediriki kusema haina makosa na inakushajihisha ujaribu kutafuta kama utapata hata moja.”

garry miller 4

Mwaka 1977, Profesa Miller (akiwa bado Mkristo) alifanya dahalo wa kidini na mwanachuoni mashuhuri wa kiislamu A h m e d Deedat. Na i l i p o t i m u 1978, baada ya kupokea dalili nyingi zaidi zioneshazo ukweli wa Ui s l amu, Professa Miller aliamua kuwa Muislamu na kuchukua jina la Abdul-Ahad likimaanisha ‘Mja wa Aliye Mmoja (yaani mja wa Mungu)’. Amefanya kazi kwa miaka kadhaa katika Chuo Kikuu cha Mafuta na Madini,Saudi Arabia na kujitolea maisha yake katika kuuhubiri Uislamu kupitia vipindi vya televisheni na mihadhara ya wazi. Gary Miller ametunga makala mbali mbali kuhusu masuala ya dini.**


** Hii ilikuwa ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho“Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant”  Kwa usomaji wa ziada tembelea www.extremelysmart.org au www.facebook.com/muerevumno “**


logompya


Search Videos

RSS Content

<

 

WhatsApp This Page Now
 

Visitors Counter

6965253
TodayToday7994
Highest 07-11-2020 : 11735
US
Guests 176

Kinga ya Muislamu

11hesn elmuslim

 

Masomo

title_5f0ca879a4b4b11126636151594665081
title_5f0ca879a4c2314547895571594665081
title_5f0ca879a4ce316545546161594665081
 

 

TARJAMA YA AL-MUNTAKHAB

title_5f0ca879c897c18617317981594665081
title_5f0ca879c8a0e5537348691594665081

HUDUMA MPYA

: 3 + 8 =

uongofu.com

Ni mtandao mpya wa ulinganizi unao funza mafunzo ya dini ya kiislamu kuambatana na Qur'ani na Sunna za Bwana Mtumeﷺ zilizo sahihi‎ kwa ufahamu wa wema walio tutangulia.

UongofuUongofu.com